27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Azam kuongeza kasi kwa JKT leo?

AZAM-FCNA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

TIMU ya soka Azam FC leo inaingia tena kibaruani kusaka pointi tatu muhimu mbele ya maafande wa JKT Ruvu, zitakazoendelea kuwapa matumaini ya kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara hatua ya lala salama.

Azam itawakaribisha wanajeshi hao wa Jeshi la Kujenga Taifa katika uwanja wake wa nyumbani wa Chamazi Complex, Dar es Salaam.

Wanalambalamba hao wanaingia uwanjani wakiwa tayari hesabu zao za ubingwa zimeanza kuvurugika, baada ya kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Simba kwenye mchezo wao uliowakutanisha mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia pointi 59 ikitofautiana kwa pointi tisa na vinara wa ligi, Yanga yenye pointi 68 huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi.

Timu hiyo itaendelea kuwakosa wachezaji wake Frank Domayo na Shomari Kapombe ambao ni majeruhi, huku Himid Mao aliyekuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu tayari amemaliza adhabu hiyo.

Akizungumzia maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo, kocha msaidizi Denis Kitambi alisema mchezo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuwa inahitaji kupata pointi.

“Mechi itakuwa ngumu lakini tunahitaji kupata pointi tatu na tumewaandaa wachezaji wetu kwa kuchukua ushindi, jana (juzi) walipumzika na leo (jana) walianza mazoezi mara mbili kwa ajili ya mchezo huu,” alisema.

Kwa upande wake, kocha msaidizi wa JKT Ruvu, Mrange Kabange, alisema wanaingia uwanjani kwa tahadhari kubwa huku wakijihakikishia hawapotezi mchezo huo, kwani wanahitaji pointi tatu ili iwakomboe katika hatari ya kushuka daraja.

“Hatuhitaji kupoteza mchezo huu, tunaingia huku tukiwa tumejiandaa kikamilifu, kwa nafasi tuliyokuwa sasa hatuhitaji kupoteza mchezo, hivyo tutapambana kuhakikisha tunakamilisha mpango wetu,” alisema.

JKT Ruvu inashika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25, maafande hao watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Tanzania Prisons wakiwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles