25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Askofu Pengo ang’atuka, nafasi yake yachukuliwa na Ruwa’ichi

Anna Potinus, Dar es Salaam

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Polycarp Pengo ameng’atuka wadhifa huo na nafasi yake imechukuliwa na Askofu Mkuu mwandamizi, Yuda Ruwa’ichi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC), Charles Kilima, Askofu Pengo ameng’atuka baada ya kuomba kustaafu majukumu ya kuliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam ombi lililoridhiwa na Baba Mtakatifu Francisko na kumteua Askofu Ruwa’ichi kushika nafasi hiyo.

Katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Miaka 75 ya kuzaliwa kwake, Askofu Pengo aliwaambia waumini wa Jimbo kuu la Dar es Salaam kwamba, anasubiria wakati wowote kumtii Baba Mtakatifu Francisko atakapomwambia kupumzika katika utume wa Kiaskofu.

Askofu Pengo ameliongoza Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa miaka 27 tangu mwaka 1992 akimpokea Askofu Laurean Rugambwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles