25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 3.6 ya watoto hawajaandikishwa shule  

watotoNA ALLY  BADI  KILWA

LICHA ya Serikali kutangaza elimu bure kuanzia elimu ya awali hadi ya sekondari, imebainika kuwa asilimia 3.6 ya watoto wote walio na umri wa kuanza shule wilayani Kilwa mkoani Lindi, hawajaandikishwa.

Hayo yameelezwa juzi na Mtafiti wa Shirika la Action Aid, Jacob Kateri, alipowasilisha ripoti ya utafiti wakati wa kikao kazi na wadau wa elimu mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai.

Akiwasilisha ripoti hiyo, Kateri alisema utafiti uliofanywa kati ya Shirika hilo na Mtandao wa Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Wilaya ya Kilwa (Kingonet), umebaini kuwapo na changamoto mbalimbali zikiwamo watoto kuendelea kuzunguka mitaani bila kuanza masomo.

Alisema kitendo cha watoto walio na umri wa kuanza shule kuendelea kubaki majumbani, kinasababisha wakose haki yao ya kupata elimu itakayowasaidia maishaini mwao.

Alivitaja baadhi ya vijiji ambavyo bado vina watoto wengi wanaozunguka mitaani bila ya kuanza kusoma ambavyo ni  Mingumbi, Nandembo na Lihimaliyao ya Kusini.

“Utafiti wetu tulioufanya shule 15, tumebaini kati ya wanafunzi wote walio na umri wa kuanza shule wapo mitaani, huku wavulana wakiwa ni wengi kuliko wasichana, kwa uwiano wa asilimia 52.4 na 47.6,” alisema Kateri.

Alisema hadi kufikia mwaka huu, watoto walioandikishwa ni asilimia 7.8, kati yao asilimia 3.5 ni wavulana na 3.3 ni wasichana.

Kwa upande wake, Ngubiagai amewaomba wadau hao wa elimu kushirikiana na watendaji wa vijiji, kata na tarafa  ili kuhakikisha asilimia ya watoto hao walio na umri wa kuanza shule ambao wapo mitaani wanaandikishwa ili waanze masomo yao.

Alisema changamoto inayoikabili idara ya elimu ya msingi ni pamoja na upungufu wa walimu 307, huku akiwataka wale wote wanaoishi nje ya vituo vya kazi kurudi mara moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles