23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

ASHA BARAKA ATAJA KINACHOIUA TWANGA PEPETA

NA JESSCA NANGAWE


MKURUGENZI wa Twanga Pepeta, Asha Baraka, amesema moja ya vitu vinavyopoteza mwelekeo wa bendi hiyo kwenye muziki wa dansi ni pamoja na muda wa kufanya matamasha kuwa mdogo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Asha alisema kitendo cha matamasha kufanyika mwisho saa 6 usiku, imekuwa moja ya changamoto kubwa inayowarudisha nyuma kwani wamekuwa wakikosa mashabiki, hivyo wanaiomba Serikali kuliangalia hilo.

Alisema tayari wamekutana katika vikao mbalimbali na kuandika barua kwa waziri mwenye dhamana ya sanaa wakimwomba kusogezwa muda angalau wa saa mbili au tatu mbele, badala ya saa sita iwe saa nane au saa tisa.

“Tulikutana na kuamua kuiomba Serikali iingilie kati suala hili kwa kuwa linatuumiza sisi kama wahusika, muda tulioomba umekwisha na tunachoangalia ni kuvuta subira na ikifika mwezi wa nne tutafanya jitihada za kumuona rais,” alisema kiongozi huyo.

Alisema moja ya mambo waliyoomba wapewe kipaumbele ni pamoja na kupewa siku mbili kwa wiki kuweza kufanya matamasha yao, huku wakiamini hayataleta madhara kwao wala kuvunja sheria za nchi.

Aliongeza pia wameandaa matamasha mbalimbali kwa ajili ya kuutangaza muziki huo ikiwemo kufanya ziara katika vyombo vya habari ambavyo ndivyo vyenye nafasi kubwa ya kurudisha heshima yao kama awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles