23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

WOLPER: UFUNDI SEREMALA UNANILIPA

NA JESSCA NANGAWE


STAA wa filamu nchini, Jackline Wolper, amesema moja ya biashara zake zinazompa furaha na kipato ni pamoja na ufundi seremala, kwa kuwa wateja kwake wamekuwa hawakauki.

Wolper alisema awali kazi hiyo ilikuwa na changamoto nyingi kwake, lakini sasa ameanza kuona matunda yake baada ya kuanza kupokea oda mbalimbali kutoka kwa wateja wake.

“Ukweli nafurahia sana hii biashara, ilinipa changamoto sana awali lakini sasa naona matunda yake, wateja wameanza kuwa wengi na hii ni kutokana na ubora wa kazi zetu, nimekuwa nahakikisha kazi tunazofanya zinakuwa na ubora ili tusiwapoteze wateja wetu,” alisema Wolper.

Msanii huyo aliongeza kuwa ni wakati sasa kwa wasanii hasa wa kike kujiongeza zaidi na kutoogopa aina ya biashara wanazofikiria kuzifanya kwa kuwa kutegemea sanaa pekee haiwezi kutimiza ndoto zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,226FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles