23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SIMULIZI YA MTANZANIA ALIYETUNUKIWA TUZO MEXICO

Na MWANDISHI WETU



ILIKUWA Mei ya miaka 50 iliyopita katika Jiji la Mexico, nchini Mexico wakati John Stephen Akhwari alipoifundisha dunia somo kwa ujasiri na ushupavu mkubwa.  Ilikuwa katika kilomita 42 ya alama wakati alipogongana na mshindani mwingine na kupata majeraha makubwa ikiwamo baya na kuvunjika goti na kuumia bega kwa kutaja machache.

Katika mchuano ambao washindani 18 kati ya 75 walimaliza mchuano, ambao Akhwari licha ya yaliyomkuta hakukata tamaa kumaliza mbio hizo.

kilomita 23 baadaye wakati giza lilipoingia na umati ukitoweka taratibu kwenye Uwanja wa Estadio Olímpico Universitario hatimaye Akhwari akaibuka katika kilomita 800 ya alama akichechemea kumaliza katika mstari wa mwisho.

Hii ilikuwa zaidi ya saa moja tangu mshindi atangazwe. Ujasiri, uvumilivu na dhamira yake iliuacha umati mdomo wazi kwa mshangao mkubwa wasiweze kuamini wanachokishuhudia hivyo kuwalazimisha wafanyakazi wa televisheni wakurupuke kurudi wasikose tukio hili la kishujaa na kihistoria.

Mtangazaji alisikika “Ni miito ya sauti kutoka ndani inayosisitiza kuendelea”.

Wakati alipouliza nini kimemfanya aendelee licha ya kuumia vibaya namna hiyo, lilikuwa jibu lake lililoishtua zaidi dunia, alijibu kuwa nchi yake haikumtuma maili 9,000 kwenda kuanza michuano, bali alitumwa kumaliza michuano.

Baadaye katika kitabu kiitwacho “The Olympic Odyssey: Rekindling the True Spirit of the Great Games” Mwandishi Phil Cousineau aliandika “ Leo tumeona mkimbiaji kijana kutoka Afrika, aliyeonesha moyo mzuri wa Kiafrika. Utendaji ambao unatoa maana ya kweli ya ushiriki michezo. Utendaji ambao unatoa maana ya neno ushujaa.
Joel Osteen na wengine wengi wasio na idadi wameendelea kutumia mfano wa Akhwari kuchochea na kutia moyo wengine. Simulizi kumhusu inatumika kama ukumbusho kwamba vikwazo vyote vinavyowekwa mbele yetu katika maisha; Ukosoaji, kujikwaa, vipindi vya afya dhaifu, kukata tamaa, kutojibiwa maombi na kile tunachokiona kama kukosa bahati.

Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas, wamejisikia fahari, kama binadamu kuibeba maana ya dhamira ya kweli na nguvu na moyo wa kibinadamu. Wakati wakisherehekea safari kuelekea juu, kupaa kuelekea vilele vipya, hakuna mtu mwingine anayekuja akilini mwao na kuwakumbusha kuhusu umuhimu wa uvumilivu na kuufikia mstari wa kumalizia mbio zaidi yako.

“Tunakushukuru na tunapenda dunia ikumbuke mchango wa michezo, Olympiki kutoka mmoja wa wale walioutoa vyema, Mtanzania mwenzetu, John Stephen Akhwari,” alisema Ben Kazora, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania, Dallas,Texas.

“Katika mwisho huu, Siku ya Tanzania 2018 mjini Dallas, Texas imekuzawadia tuzo ya “TUNU ADIMU, Tuzo hii ni kwa watu wachache ambao wanaweka masilahi ya Taifa kwanza na wanafanya hivyo kwa fahari hadi mwisho wa safari yao.

“Simulizi zako zinaendelea kuchochea vizazi na tunaheshimu kwa mchango wako wakati ukiiwakilisha Tanzania kwa heshima katika jukwaa la dunia,” alisema Kazora.

 

Historia

John Stephen Akhwari alizaliwa Machi 27, 1938 katika Kijiji cha KHADAY Kata ya SANU, Tarafa ya Endagikot, Wilaya ya Mbulu.

 

Elimu

Alianza elimu ya Msingi mwaka 1952 hadi mwaka 1956 katika Shule ya Msingi Muslim School na baadaye mwaka 1959 alijiunga Middle School hai mwaka 1962 Middle Schoo ya Endagikot.

 

Michezo

Alianza safari yake ya michezo mwaka 1958 hadi 1976 alipostaafu rasmi.

Mwaka 1958 alishiriki mbio za kiwilaya hadi mwaka 1959 ilikuwa ni mbio za kilomita 15 na kumaliza akiwa mtu wa 40 kati ya watu 70 na kuzawadia soda ya Coca Cola.

Mwaka 1959 alishiriki mbio za kilomita 10 na kushika nafasi ya kwanza kati ya 90 na kuzawadiwa blanketi, taa ya chemli na chupa ya Zinzano na Paundi 20 ya Uingereza.

Mwaka 1960 alishiriki michezo ya mkoa ya maili tatu na kushika nafasi ya kwanza kati ya watu wanane huku michuano hiyo ikiwa haina zawadi na maka 1961 alishiriki mashindano ya Middle School Karatu, Endagikot na Dareda ya maili tatu na maili sita na kushika nafasi ya kwanza.

Mwaka 1962 alishiriki mashindano ya kanda ya maili moja na kushika nafasi ya kwanza na mwaka huo huo alishiriki mashindano ya Taifa ya maili tatu na sita yaliyofanyika Dar es Salaam na kushika nafasi ya kwanza.

Mwaka huo huo tena akashiriki mashindano ya Marathon ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Nairobi Kenya na kushika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa kikombe.

Mwaka huo huo tena wa 1962 alishiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola ya kilomita 42 yaliyofanyika West Australia na kushika nafasi ya sita na baadaye mwaka huo huo kushiriki michezo ya kirafiki ya maili tatu iliyofanyika Sri Lanka Celon na kushika nafasi ya pili.

Mwaka 1963 alishiriki mashindano ya Kimataifa ya kilomita 42 yaliyofanyika Ugiriki na kushika nafasi ya pili na kupata zawadi ya cheti, kikombe, jani isiyokauka na Dola za Kimarekani 1,000.

Mwaka 1967 alishiriki mashindano ya kilomita 42 ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Kampala- Uganda na kupata zawai ya kikombe.

Mwaka 1968 alipata mafunzo ya mwezi mmoja ya Skauti yaliyofanyika Loltoktok nchini Kenya na kupanda Mlima Kilimanjaro. Ndipo mwaka huo huo, Oktoba 20, alishiriki mashindano ya Olimpiki ya kilomita 42 Jijini Mexico. Wakimbiaji wakiwa 75 huku Akhwari akishika nafasi ya 57 baada ya kuumia kutokana na hali ya hewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles