30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi za kiraia zatakiwa kuhamasisha sensa

NA RAMADHAN HASSAN, Dodoma

KAMISAA wa Sensa na Makazi nchini, Anne Makinda amezitaka asasi za kiraia nchini kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi iliyopagwa  kufanyika   Agosti mwakani.

Akizungumza leo Oktoba 27,2021 wakati akitoa mada ya uelimishaji na uhamasishaji wa zoezi la sensa na makazi kwa asasi za kiraia katika mkutano wa wiki ya Azaki mkoani Dodoma,kamisaa huyo ameziomba asasi hizo kupaza sauti juu ya umuhimu wa kuhesabiwa.

 “Tunawaomba mzungumze masuala ya kuhesabiwa,  nchi kubwa hii wengine hawajui wapo wapi. Sensa ni muhimu na inafanyika kila baada ya miaka kumi,nyinyi watu wa Azaki ni wadau namba moja ,tunatakiwa kutoka kwenye uchumi wa kati tufanane na wenzetu.

 “Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum,kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi. 

“Kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi. Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwamo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo,”amesema.

Makinda amesema sensa hiyo itazingatia  taarifa za idadi ya watu na husaidia  katika mamlaka za wilaya katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ambayo huakisi matakwa ya watu katika ngazi husika na kusaidia kwenye uwiano wa mgawanyo wa rasilimalimali.

Kwa upande wake,Mtakwimu Mwandamizi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu,David Mwaipopo  amesema sensa ya mwaka 2022 kama zilivyo zilizopita itatumia aina mbili kuu za madodoso ambazo ni dodoso refu litakalotumika kuhoji asilimia 30 ya maeneo yote ya kuhesabia watu na dodoso fupi litakalotumika kuhoji kwenye asilimia 70 ya maeneo yote ya kuhesabia watu.

Ameyataja madodoso mengine kuwa ni  la taasisi ambalo ni mahsusi kwa ajili ya wasafiri, waliolala mahotelini, nyumba za wageni, na waliolazwa hospitalini na dodoso la wasio na makazi maalum kwa watu wote wanaolala maeneo yasiyo rasmi, kwenye baraza za majengo,madaraja na maeneo mengine.

“Utekelezaji wa sensa ya watu na makazi hufanyika katika awamu kuu tatu kuu ambazo ni kipindi kabla ya kuhesabu watu, wakati wa kuhesabu watu na kipindi baada ya kuhesabu watu,”amesisitiza.

Mtakwimu huyo amefafanua maswali yatakayoulizwa wakati wa sensa  kuwa moduli kumi na nne zitatumika kukusanya taarifa za watu na makazi yao nchi nzima.

“Maswali hayo ni tarifa za kidemografia (umri, jinsi, uhusiano, hali ya ndoa, uraia, maswali yanayohusu ulemavu, tarifa za elimu, maswali ya uhamaji, pamoja na taarifa za watanzania wanaoishi nje ya nchi.

“Mengine ni maswali kuhusu umiliki wa nyaraka za kitaifa (vitambulisho vya NIDA, Mzanzibari mkazi, cheti cha kuzaliwa, hati ya kusafiria, na leseni ya udereva), shughuli za kiuchumi na umiliki wa ardhi na taarifa za TEHAMA,”amesema.

Mengine ni taarifa za uzazi na vifo vilivyotokea ndani ya kaya,vifo vitokanavyo na uzazi,hali ya nyumba za kuishi na umiliki wa rasilimali mbalimbali,maswali ya kilimo na mifugo pamoja na mifuko ya hifadhi ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles