24.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni yatakiwa kuanza uchimbaji madini haraka

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

BAADA ya Kampuni ya Tembo Nickel Corporation Limited kupatiwa leseni ya uchimbaji mkubwa wa madini ya Nickel, Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka kampuni hiyo kuanza shughuli ya uchimbaji mara moja huku akidai uwekezaji huo ni muhimu na una faida kwa Nchi.

Akizungumza leo Oktoba 27,2021 jijini Dodoma  wakati wa utoaji wa leseni kwa kampuni hiyo na uzinduzi wa taarifa ya uhamasishaji ,uwazi na uwajibikaji  katika rasilimali madini,mafuta na gesi asilia ya mwaka 2018-2019, Ndugai amesema Watanzania ni watu wema.

“Watanzania ni watu wema sana mkafanye kazi kama leseni yenu inavyosema muanze shughuli mara moja na niwahakikishieni kwa niaba ya Serikali mtapata kila aina ya ushirikiano pamoja na kwamba shughuli zenu zinahusisha Wizara nyingi sana lakini naamini kupitia Wizara hii mtapata ushirikiano,”amesema.

Spika Ndugai ambaye ni Mbunge wa Kongwa amesema uwekezaji huo una faida nyingi kwa nchi pamoja na wakazi wa Ngára mkoani Kagera kwani utatoa ajira na kila wizara itaguswa na uwekezaji huo.

Amezitaka wizara kujipanga ili kuhakikisha mambo yanaenda vizuri huku akidai Bunge litaisaidia kamati ya Nishati na Madini iweze kufanya ufuatiliaji wa uwekezaji wa kampuni hiyo.

Aidha Spika huyo amewataka watanzania ambao watapa nafasi ya kufanya kazi katika kampuni hiyo kufanya kwa weledi pamoja na kutanguliza uzalendo mbele.

“Ndugu zetu wa Tembo Nickel Corporation Limited hasa ninyi watanzania ambao mpo ndani ya kampuni hii ya ubia na ndugu zetu ambao mpo humu ndani kawajibikeni msituangushe hatujawatuma huko kwenda kulala.

Aidha amewataka wakazi wa Ng’ara kuziwahi fursa mbalimbali ambazo zitajitokeza huku akisisitiza wakichelewa watu kutoka katika maeneo mengine wataziwahi.

Kwa upande wake,Waziri wa Madini,Doto Biteko ameitaka kampuni hiyo baada ya kupewa leseni ianze zoezi la uchimbaji maji mara moja.

Naye,Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Januari Makamba amesema wamejipanga kuhakikisha umeme wa kutosha unapatikana katika eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles