22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Halopesa yazindua “Play &Win’’

Na Iman Nathaniel, Dar es Salaam

KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Halotel kupitia huduma yake ya HaloPesa,imezindua huduma nyingine ya kujishindia zawadi mbalimbali iliyopewa jina la  ‘Play & Win kwa wateja wake nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 27, 2021, jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi  Mtendaji wa HaloPesa, Magesa Wandwi, amesema Play& Win ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka ya kufikisha thamani  ya maisha ya wateja wake.

‘’Tuna uhakika kwamba wateja wa HaloPesa watafurahia huduma yetu na ambao bado hawajatumia HaloPesa watajiunga ili kufurahia huduma hii,”amesema.

Kwa upande wa mkuu wa huduma na mahusiano wa kwa wateja wa Dunia Investment ambaye ni mbia wa huduma ya  hiyo,Kobus Schoeman, amesema kuwa michezo na burudani ni sehemu ya asili ya utamaduni wa Afrika ambapo kwa inagusa  maisha.

Naye Ofisa wa bidhaa na masoko wa HaloPesa ,Roxana Kadio  amesema kuwa  katika kampeni hiyo mteja atapata halopointi za bure kulingana na aina ya miamala .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles