28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Arsenal kuikaribisha Liverpool Ligi Kuu

arsenal vs liverpoolLONDON, ENGLAND

RATIBA ya michuano ya Ligi Kuu nchini England imetoka jana ambapo mabingwa Leicester City wataanzia ugenini dhidi ya Hull City, wakati huo Arsenal wakiwa nyumbani na kuwakaribisha majogoo wa jijini Liverpool.

Michuano hiyo inatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti 13 mwaka huu. Kocha mpya wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, ataiongoza timu yake katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bournemouth ugenini.

Wakati huo kocha mwingine mpya wa Manchester City, Pep Guardiola, ataanza kuonja ladha ya michuano ya England katika mchezo wake dhidi ya Sunderland kwenye uwanja wa Etihad.

Wakati huo Chelsea itashuka dimbani ikiwa na kocha wao mpya, Antonio Conte, ambapo watapambana na West Ham United kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

Katika michezo hiyo ya awali, mchezo ambao unaangaliwa sana wiki hiyo ni kati ya Arsenal dhidi ya Liverpool.

Michezo mingine ambayo itapigwa wiki hiyo ni Burnley dhidi ya Swansea City, Crystal Palace dhidi ya West Bromwich, huku Everton wakipambana na Tottenham, Middlesbrough na Stoke City wakati huo Southampton ikicheza na Watford.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles