23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ronaldo ashindwa kuibeba Ureno

Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo

MARSEILLE, UFARANSA

NYOTA wa timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo, ameshindwa kuisaidia timu yake katika michuano ya Kombe la Euro 2016 na kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya wapinzani wao Iceland.

Iceland hawakupewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo mbele ya mastaa wengi wa Ureno, hata hivyo Iceland walikuwa wanacheza mchezo wao wa kwanza wa mashindano makubwa Ulaya.

Ureno walikuwa wa kwanza kupata bao ambalo lilifungwa na mshambuliaji wao Nani, lakini Iceland wakapambana na kusawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wao, Birkir Bjarnason.

Katika mchezo huo, Ronaldo alionekana mara kwa mara akijaribu kupambana lakini hakufanikiwa kufanya lolote kama ilivyodhaniwa na wapenzi wengi wa soka.

Ronaldo ameingia kwenye mashindano hayo akiwa ametoka kuipa klabu yake ya Real Madrid ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa bao lake la mwisho katika mikwaju ya penalti dhidi ya Atletico Madrid.

Katika mchezo huo, mchezaji wa timu ya Ureno, Renato Sanches, ameweka rekodi ya kucheza huku akiwa na umri mdogo zaidi kwenye timu hiyo katika mashindano makubwa akiwa na miaka 18 na siku 301, wakati huo Cristiano Ronaldo  aliwahi kucheza akiwa na miaka 19 na siku 128.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles