23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Andy Cole asumbuliwa na figo

andy-coleMANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Manchester United, Andy Cole, anasumbuliwa na ugonjwa wa figo, ambao unamsababishia kupungua uzito kwa asilimia 20.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 44, alianza kusumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka jana, lakini kwa sasa hali inaonekana kuzidi na kumsababishia mwonekano wake kuanza kubadilika kutokana na figo kushindwa kufanya kazi.

“Wakati natarajia kustaafu soka niliwaambia wanangu kwamba sitakubali mwili wangu uzidi hapa nilipo na kuongezeka uzito, kwa kuwa nilijua kwamba nitajiachia, hasa kwa kunywa na kula.

“Angalia kwa sasa mwili wangu ulivyobadilika na nimepata ujumbe mbalimbali kutokana na mabadiliko hayo, lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti tena, maana mwili unapungua na watu wanashangaa, lakini hii yote ni kutokana na figo kushindwa kufanya kazi,” alisema Cole.

Nyota huyo alicheza jumla ya michezo 624 katika klabu za nchini England na kufanikiwa kushinda mabao 271 katika klabu za United, Blackburn na Newcastle United.

Katika klabu ya United, mchezaji huyo alifanikiwa kucheza michezo 275 na kufunga mabao 121, na kuisaidia klabu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi mara tano na Ligi ya Mabingwa akiwa chini ya kocha Sir Alex Ferguson

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles