Ronaldinho ahangaika kutafuta timu

0
571

ronadinhoPORTO ALEGRE, BRAZIL

NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya Taifa ya Brazil, Ronaldinho Moreira, amesema kwa sasa anatafuta timu ya kuitumikia hili aweze kumalizia soka lake.

Mchezaji huyo alikuwa anakipiga katika klabu ya Fluminense ya nchini Brazil, lakini amemaliza mkataba wake na sasa anatafuta timu ya kuitumikia hili aweze kumalizia soka lake.

Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, amesema lengo lake ni kupata klabu kubwa ambayo inashiriki michuano mbalimbali Ulaya.

“Kila kitu kina wakati wake, ninaamini nitapata timu ya kuitumikia, lakini lengo langu ni kuipata ambayo itakuwa inashiriki michuano mbalimbali barani Ulaya.

“Uwezo bado ninao na ndiyo maana kaka yangu anahangaika kwa ajili ya kunitafutia timu ambayo naweza kwenda kumalizia soka langu, lakini ninavyojiona naweza kucheza soka kwa miaka mitano mbele,” alisema Ronaldinho.

Mchezaji huyo kwa sasa anaonekana katika viwanja mbalimbali vya starehe nchini Brazil, huku akiwa na warembo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here