28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

AMANDA ATUMIA SEKUNDE 48 KUSHINDA KO

LAS VEGAS, MAREKANI


3bb9dd5300000578-4077576-image-a-45_1483164246603BINGWA wa mchezo wa ngumi kwa wanawake, Ronda Rousey, amechezea kichapo katika raundi ya kwanza sekunde ya 48 dhidi ya mpinzani wake, Amanda Nunes.

Ronda alikuwa nje ya uwanja katika michuano hiyo ya UFC kwa muda wa miezi 13 tangu Novemba 2015, baada ya kusimamishwa kutokana na uvunjaji wa sheria za mchezo huo.

Lakini katika mchezo huo ambao umepigwa Desemba 30 ulikuwa wa kwanza kwake tangu adhabu yake ilipokwisha, lakini alijikuta akichezea kichapo ndani ya dakika moja na pambano likamalizikia hapo.

Rousey amedai kuwa, ni pambano ambalo lilikuwa linafunga mwaka 2016 na kuukaribisha 2017, hivyo hawezi kulisahau kutokana na kupata ubingwa wa UFC kwa urahisi.

“Nilijua kwamba pambano litakuwa gumu sana kutokana na uwezo wa mpinzani wangu, japokuwa hakuwa kwenye mchezo kwa muda mrefu, lakini niliamini angeweza kunisumbua kwa kuwa bado alikuwa anaendelea na mazoezi.

“Naweza kusema kuwa, ni pambano ambalo nitalikumbuka kwa kuwa nilitumia muda mfupi kuweza kushinda, hivyo ni historia kwangu kwa kuwa ni ndani ya dakika moja pambano likamalizika.

“Ni furaha kubwa kwangu kumaliza mwaka 2016 huku pambano langu la mwisho nikishinda kwa KO, ninaamini ni dalili nzuri kwa mwaka 2017 kufanya makubwa zaidi,” alisema Amanda

Kwa upande wake Rousey, amedai kuwa mpinzani wake alikuwa na maandalizi mazuri na ndiyo maana ameweza kushinda mapema, lakini atajipanga kuhakikisha anafanya makubwa 2017.

“Nimemaliza vibaya 2016 kutokana na maandilizi yangu kuwa mabaya, lakini ninaamini 2017 nitahakikisha ninarudisha heshima yangu na kuwapa furaha mashabiki wangu.

“Nilikuwa nje ya uwanja kwa miezi 13, kitu ambacho kimenifanya nipoteze mambo mengi, lakini kwa kuwa nimerudi kila kitu kitakuwa sawa kama ilivyo awali,” alisema Rousey.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles