Na VALERY KIYUNGU- DAR ES SALAAM
MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa taarabu nchini, Ally Star, ameweka wazi kwamba muziki huo upo hatarini kutoweka endapo juhudi za kuunasua hazitachukuliwa.
Ally ambaye ni msanii wa kundi la sanaa la Tanzania One Theatre (TOT), alisema kiwango cha muziki kimeshuka ikilinganishwa na miaka ya 1980.
Alisema muziki wa taarabu hivi sasa umekutana na changamoto nyingi kutokana na kuibuka kwa aina mbalimbali za muziki ikiwemo Bongo Fleva na Singeli.
“Kwa sasa mimi nikipanda jukwaani nitabebwa na jina langu lakini kwa kutegemea majina tu hatutafika mbali, inabidi tujitahidi turudi kule tulipotoka katika muziki wa taarabu,” alisisitiza.
Ally Star aliwahi kutamba na nyimbo ‘Natanga na njia’ na ‘Kala hasara’.