27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ALLY STAR: TAARABU ITAKUFA TUSIPOISAIDIA

Na VALERY KIYUNGU- DAR ES SALAAM


aliMWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa taarabu nchini, Ally Star, ameweka wazi kwamba muziki huo upo hatarini kutoweka endapo juhudi za kuunasua hazitachukuliwa.

Ally ambaye ni msanii wa kundi la sanaa la Tanzania One Theatre (TOT), alisema kiwango cha muziki kimeshuka ikilinganishwa na miaka ya 1980.

Alisema muziki wa taarabu hivi sasa umekutana na changamoto nyingi kutokana na kuibuka kwa aina mbalimbali za muziki ikiwemo Bongo Fleva na Singeli.

“Kwa sasa mimi nikipanda jukwaani nitabebwa na jina langu lakini kwa kutegemea majina tu hatutafika mbali, inabidi tujitahidi turudi kule tulipotoka katika muziki wa taarabu,” alisisitiza.

Ally Star aliwahi kutamba na nyimbo ‘Natanga na njia’ na ‘Kala hasara’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles