22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Alicia Keys ambeba DJ wa Kenya

Alicia Keys
Alicia Keys

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Alicia Keys, amemfanya Peter Kerre kuwa maarufu kwa jina la DJ Xpect, kuzidi kuwa na jina kubwa baada ya wimbo ambao alifanya na DJ huyo kupigiwa kura na kushinda.

Alicia ambaye anatamba na wimbo wake wa ‘In common’, aliamua kuufanyia remix na DJ watatu akiwa pamoja na mshindi wa tuzo ya BET kutoka nchini Afrika Kusini, Black Coffee. Hivyo msanii huyo aliziweka remix hizo kwenye akaunti yake ya Twitter na kuwataka mashabiki wapige kura na DJ Xpect akaibuka mshindi.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la nchini Kenya, DJ Xpect, ambaye makazi yake kwa sasa ni nchini Marekani, aliorodheshwa Alicia Keys kwenye kampuni ya Sony Records tangu Juni mwaka huu.

DJ Xpect amewashukuru mashabiki kwa kukubali kazi zake na kuufanya wimbo huo alioufanya na Alicia kuzidi kumpa jina kubwa duniani

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles