Rihanna ahofia virusi vya Zika Colombia

Robyn Fenty ‘Rihanna
Robyn Fenty ‘Rihanna
Robyn Fenty ‘Rihanna

BOGOTA, COLOMBIA

MKALI wa muziki wa Pop nchini Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’, amesitisha ziara yake nchini Colombia kwa kuhofia kuambukizwa virusi vya Zika.

Waandaaji wa tamasha la Lollapalooza nchini Colombia, wamepigwa na butwaa baada ya msanii huyo kuwapa taarifa kwamba hataweza kwenda kwenye tamasha hilo kutokana na kuhofia kuambukizwa virusi hivyo.

Inadaiwa kwamba tayari maelfu ya mashabiki walikuwa wamenunua tiketi zao kwa ajili ya kwenda kumshuhudia msanii huyo.

”Baada ya kujiondoa kwa nyota wa muziki wa Pop, Rihanna, hatuna budi kufutilia mbali tamasha zima, hata hivyo tunawaomba radhi mashabiki wetu kwa tukio hilo na tungependa kuwahakikishia kuwalipa gharama za tiketi zilizonunuliwa,” alisema Meneja wa tamasha hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here