22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Aguero atangaza kuondoka Man City

sergio-aguero-manchester-city_3358974MANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester City, Sergio Aguero, amesema kwamba anatarajia kuondoka katika klabu hiyo baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Nyota huyo wa mabao mwenye umri wa miaka 27, amedai kwamba baada ya kuondoka katika klabu hiyo atarudi nchini Argentina kwenye klabu ya Independiente, japokuwa mkataba wake ukitarajiwa kumalizika 2019.

Aguero alisaini mkataba mpya na klabu hiyo wa miaka mitano tangu 2014 hadi 2019, lakini mchezaji huyo ameweka wazi kwamba baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia 2018 atarudi nchini Argentina kwa ajili ya kucheza ligi ya huko.

“Miezi michache iliyopita mambo mengi yalikuwa yanazungumziwa juu ya mkataba wangu, lakini nilikuwa kimya ila kwa sasa naona bora niweke wazi kwamba baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nitaondoka Man City na kurudi katika klabu ya Independiente.

“Hapa Man City ninaamini wanafanya makubwa kwa ajili yangu, wamekuwa wazi kuniambia kila kitu hata kama nataka kuondoka hawana tatizo na sasa ni muda wangu wa kuweka wazi kwamba nitaondoka kutoka mji wa Manchester hadi Avellaneda.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles