25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Van Persie aachwa timu ya Taifa

rvpAMSTERDAM, UHOLANZI

NYOTA wa zamani wa Manchester United, Robin van Persie, ameachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uholanzi kinachotarajia kucheza dhidi ya Ufaransa na England katika michezo ya kirafiki.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, kwa sasa anakipiga katika klabu ya Fenerbahce, anaongoza katika historia ya kupachika mabao katika timu ya Taifa huku akiwa na mabao 50 kati ya michezo 101 aliyocheza.

Lakini baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu michuano ya Euro 2016, kocha wa timu hiyo Danny Blind, ameamua kuchukua wachezaji wengine ambao ni damu changa.

Wachezaji wengine ambao wameachwa katika kikosi hicho ni pamoja na Van der Wiel na Maarten Stekelenburg.

Wakati huo nafasi ya Van Persier ikichukuliwa na nyota wa klabu ya AZ Alkmaar, Vincent Janssen mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa ana jumla ya mabao 10 katika klabu hiyo tangu Januari mwaka huu. 

Baadhi ya wachezaji wengine ambao wameitwa kikosini ni pamoja na Memphis Depay, Daley Blind, Arjen Robben, Wesley Sneijder, Virgil van Dijk, Daryl Janmaat, Ibrahim Afellay, Georgino Wijnaldum na wengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles