23.3 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Agizo la Rais Magufuli latekelezwa Muhumbili

mpokiNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubysia,  amewaongoza watumishi wa wizara hiyo kuhamisha vyombo kutoka kwenye jengo la afya ya uzazi na mtoto lililoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Wizara imechukua hatua hiyo baada ya kutolewa agizo na Rais Dk. John Magufuli alilotoa juzi kwenye mkutano wake na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais Magufuli aliiagiza wizara kuhama katika jengo hilo ili kupisha uongozi wa Muhimbili uweze kulitumia kama wodi ya wazazi.

Agizo hilo alilitoa baada ya kutembelea wodi ya wazazi na kukuta wajawazito wakiwa wamelala chini ili wapatiwe huduma.

Akizungumza na MTANZANIA, Dk. Ulisubsya, alisema walianza kuhamisha vifaa vilivyokuwa ndani ya jengo hilo mapema juzi asubuhi.

“Tulianza kuhama tangu juzi, naamini hadi kufikia leo (jana) jioni tutakuwa tumemaliza kuhamisha vifaa vyetu ili Muhimbili wahamie na tayari wameanza kufanya usafi kwenye baadhi ya vyumba,” alisema.

Alisema jengo hilo lilijengwa na wizara Novemba 11, mwaka 1994 na kwamba lilikuwa na watumishi 63.

“Watumishi hawa ni wengi hatuwezi kwenda kuwaweka wote pale wizarani, hivyo tutawasambaza kwenye vitengo vingine vilivyoko chini yetu ikiwamo Tume ya Kudhibiti Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (Tacaids), Taasisi ya Saratani Ocean Road, Ofisi ya Mpango wa Chanjo iliyoko Mabibo na Bohari Kuu ya Dawa (MSD),” alisema.

Fatuma Mohamed ambaye ni mmoja wa wajawazito aliyelazwa hospitalini hapo,  alisema wamefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kwani itasaidia kuondoa changamoto ya kulala chini wakiwa wanasubiri huduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles