24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Meya Kinondoni awaahidi bodaboda Sh milioni 1

Boniphace-JacobJOHANES RESPICHIUS NA MANENO SELANYIKA DAR ES SALAAM

MEYA wa Manispaa ya Kinondoni, Boniphace Jacob ameahidi kukipatia Sh milioni moja Kikundi cha Madereva wa pikipiki maarufu ‘bodaboda’ wa Kata ya Manzese (MABOA) kwa ajili usajili wa kudumu.

Jacob alitoa ahadi hiyo alipokutana na baadhi ya wanachama pamoja na viongozi wa MABOA mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

Alisema licha ya kiasi hicho cha fedha atatoa sare zitakazowatambulisha ikiwa ni pamoja na makoti ya kuakisi mwanga (reflector) na fulana kwa ajili ya usalama mahali pa kazi.

“Nitajitahidi kushirikiana nanyi katika kila jambo lakini kitu cha msingi naomba mfuate sheria za barabarani ili kuepuka migogoro na Jeshi la Polisi,” alisema Jacob.

Aidha aliwataka wanachama wa MABOA kuwa na umoja katika kila tatizo litakalompata mmoja wao na kuhakikisha haki inapatikana.

Naye Katibu wa MABOA, Ibrahim Said alisema lengo lao ni kuwafanya madereva hao waamini kuwa bodaboda ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Alisema kikundi hicho kina wanachama zaidi ya 1,000 na kwamba wako katika hatua za mwisho katika kukisajili hivyo fedha iliyotolewa na Meya huyo itawawezesha kuwaharakishia kufanya usajili huo mapema.

“Kazi yoyote inahitaji kufuata sheria ni lazima madereva wote wanatakiwa kuzifuata na jambo kubwa linalohitajika ni ushirikiano wa madereva na vyombo vya ulinzi na usalama.

“Tunataka tuondoe dhana iliyojengeka kwamba madereva wa bodaboda wana uhasama na vyombo vya ulinzi na usalama hivyo tunahitaji kutoka huko ili kuweza kushirikiana kwa pamoja,” alisema Said.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles