26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

ADELE: KAENI TAYARI KWA NDOA YANGU

LONDON, ENGLAND


 

adeleNYOTA wa muziki nchini Uingereza ambaye ametamba na wimbo wake wa ‘Hello’, Adele Adkins, amewataka mashabiki wake kusubiri ndoa yake mapema mwaka huu.

Msanii huyo ambaye alivishwa pete tangu Oktoba mwaka jana na mpenzi wake ambaye ameishi naye kwa miaka mitano, Simon Konecki, wamepanga kufunga ndoa mwaka huu.

Wawili hao walitoa tangazo mwishoni mwa mwaka jana kwamba wanatarajia kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini wamedai tangazo hilo limewekwa kwa muda mfupi, hivyo wamesitisha kufanyika Januari lakini wamedai itakuwa mapema mwaka huu.

“Ni mwaka ambao tulikuwa tunausubiri kwa upande wangu na Konecki, tulikuwa na lengo la kufunga ndoa Januari mwaka huu, lakini tunasogeza mbele kidogo ila itakuwa mapema mwaka huu, watu wakae tayari kwa sherehe hiyo,” aliandika Adele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles