30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

CHRIS BROWN AMWOMBA RADHI KARRUECHE

NEW YORK, MAREKANI


chris-brown-and-karrueche-tranMKALI wa muziki wa RnB nchini Marekani, Chris Brown, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumwomba radhi mpenzi wake wa zamani, Karrueche Tran.

Uhusiano wa wawili hao ulivunjika tangu Machi 2015, baada ya msanii huyo kuletewa mtoto wa miezi tisa ambaye alimpa jina la Royalty, mtoto huyo alimpata na mrembo mwingine ambaye alijulikana kwa jina la Nia Guzmann.

Tangu Chris aachane na mrembo huyo, amedaiwa kutoka na mwanamitindo Krista Santiago, lakini cha kushangaza msanii huyo amemwomba radhi Karrueche.

“Nilikuzoea, tulikuwa wote sehemu mbalimbali, naomba tuyasahau hayo,” aliandika msanii huyo baada ya kuiposti picha ya mrembo huyo.

Hata hivyo, maneno ya msanii huyo yanadaiwa kumweka katika wakati mgumu kwa mpenzi wake wa sasa, Krista.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles