Na Jeremia Erenest, Dar es Salaam
Wabunifu zaidi ya 10 wanatarajiwa kuonyesha mavazi katika tamasha la Runwaybay Fashion Week msimu wa kwanza lenye lengo la kuamsha Utalii wa wa Zanzibar.
Tamasha hilo litafanayika kwa muda wa siku tatu mfululizo katika maeno tofauti ya wazi kisiwani humo kuanzia Desemba 19 mpaka 21, likiwa na kaulimbiu ya ‘Ndoto yangu, Kipaji changu, Maisha yangu’.
Akizungumza na wandishi wa habari mratibu wa onyesho hilo, Waiz Waiz designer amesema maandalizi yapo katika hatua za mwisho na wanamitindo wamesha anza kufanya mazoezi ya muondoko.
“Tumejipanga vizuri kufanikisha shoo hii ambayo haijawahi kufanyika hapa nchini lengo letu kuonyesha utalii wa Zanzibari, ambao wengi bado hawajaufaham vizuri teari wanamitindo wapo katika hoteli ya Marumaru wakijifua kwa ajili ya jukwaa hili,” amesema Waiz.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wabunifu wakongwe wamejisajili kwa ajili tamaha hilo akiwemo mama wa mitindo Asia Idarous, Adam fashion, Kasikana, Enjoy Masai, DulaTailor, Waiz designer, Tngazy, Shey Styles hawa wapo Tangzanyika na Zanzibari.
Shoo hiyo itafanyika Kendwa Rock hotel, Mizingani Seafront kisha itahitimishwa The loop hotel ambapo kutakuwa na utoaji tuzo na vyeti kwa wabunifu, wanamitindo na wadau wa tasnia ya mitindo nchini na nje ya nchi.