21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Waondoeni madarakani wanaong’ang’ania madaraka-Singo

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Mkurugenzi wa Michezo nchini, Yusuphu Singo ameliagiza Baraza la Michezo nchini (BMT) kuwaondoa madarakani viongozi wa vyama vya michezo wanang’ang’ania madaraka bila kufuata Katiba.

Akizungumza leo Desemba 12 mwaka huu katika mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Mkurugenzi huyo wa michezo amesema Serikali imeanza kutafsiri kwa vitendo kauli ya Rais, DK. John Magufuli ya kutaka sekta ya michezo kuboreshwa.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi wa vyama vyote vya michezo nchini, pamoja na baadhi ya wanamichezo waliowahi kufanya vizuri na kushiriki Mashindano mbalimbali ya Kimataifa.

Mkurugenzi huyo ameliagiza Baraza la Michezo nchini kuwaondoa viongozi ambao wanang’ang’ania madarakani bila kufuata Katiba.

“Nawaagiza BMT mzaha sasa umepitwa na wakati viongozi hawataki kuondoka muwaondoe,nendeni vizuri,viongozi ambao hamtaki vyama ni kwa niaba ya Watanzania tu. Tunatarajia kutoka sehemu moja kwenda nyingine Tennis nawapongeza Sana hatutaki kusikia mnalalamikiana,”amesema Singo.

Pia, amevitaka vyama hivyo kuhakikisha vinaendeleza michezo kama ilani ya uchaguzi inavyotaka.

“Sasa Mheshimiwa Rais anasema Watanzania wanataka ushindi,ndugu zangu tuhakikishe tunaendeleza michezo hata ilani ya uchaguzi inalizungumzia hilo. Sisi kama Serikali tumeanza kutafsiri maelekeazo ya Rais na nyie viongozi nendeni mkatafsiri mazoe yamekwisha,hamuheshimu hata Katiba zenu, ninaomba kila mmoja wenu mtakaporudi jipangeni,”amesema Singo.

Katika hatua nyingine Singo amesema Desemba 19 mwaka huu,Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa anatarajia kukutana na wadau wa michezo vikiwemo vyama vya michezo kumzungumzia mpango wa Taifa wa michezo.

Hivyo amevitaka vyama hivyo kupeleka viongozi sahihi na sio kutuma Wawakilishi.

“Hili ni very serious nitakuwa na mkutano Tarehe 19 kutakuwa na mkutano wa wadau tunaongelea mpango wa Taifa wa kuendeleza michezo,nawaomba mje,msitume wawakilishi,”amesema Singo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles