28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Wakufunzi wa vyuo watakiwa kuwa wabunifu

Na Ramadhan Hassan, Dodoma                   

Walimu wa Vyuo Vikuu nchini wametakiwa kuwa wabunifu katika ufundishaji wao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawapa mbinu sahihi  wanafunzi kuweza  kujitegemea katika maisha yao.

Hayo yalielezwa jana Jijini hapa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Profesa Davis Mwamfupe wakati akizungumza katika kongamano la taaluma liloandaliwa na Chuo Kikuu cha St John cha Jijini hapa.k

Kongamano lilikuwa na mada zilizohusu mchakato wa Vyuo Vikuu katika kuendeleza Technolojia na kuhamasisha uvumbuzi  wa mabadiliko ya kiuchumi  na maendeleo endelevu Tanzania.

Mbali na kongamao hilo pia Chuo hicho kilitoa zawadi na cheti kwa wanafunzi waliofanya vizuri kwa ujumla katika ngazi ya Astashahada, Stashaha, Shahada katika masomo mbalimbali.

Prof. Mwamfupe alisema walimu wanatakiwa kuwa wabunifu katika ufundishaji wao ikiwa ni pamoja na kuwa tofauti na ufundishaji wa miaka ya zamani huku akiwataka kutumia zaidi teknolojia katika ufundishaji.

“Tuna jukumu la kuangalia njia za kufundishia sio wanafunzi wanatoka hapa huko wanapoenda kila mara wanauliza ametoka wapi huyu.Kubwa wanafunzi wanaiga kwetu sisi walimu tunatakiwa kuwa makini na aina ya ufundishaji huna ubunifu wowote lazima yeye atoke hana kitu,”alisema Prof Mwafupe.

Meya huyo wa Jiji la Dodoma ambaye pia amewahi kufundisha Vyuo kadhaa kikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) alisema ni vizuri wanafunzi wakafundishwa jinsi ya kutengeneza sera ambapo amedai ufundishaji wa baadhi ya walimu unawafanya wanafunzi  wategemee mitandao.

Pia,alisema baadhi ya ufundishaji wa walimu wa kuwajazia mambo  mengi kwa wakati mmoja kunawafanya baadhi ya wanafunzi washindwe kuelewa.

“Mwanafunzi kapata jibu tunatakiwa tuulize sasa hilo jibu kalipataje hapo ndio itatusaidia maana jibu anaweza hata kubaatisha.Hatuwezi kupata mtoto kwa kama tulivyokuwa tukifikiria juzi,jana na leo,”alisema.

Naye, Mhadhiri wa Chuo hicho kutokea Idara ya Kiswahili Dk.Shadidu Ndossa alisema kwa sasa teknolojia ipo kila mahali na ni kitu muhimu  hivyo  Vyuo vikuu  vinatakiwa kuwa na sauti moja kuwaunganisha watu wote ili jamii iweze  kupata manufaa.

“Mfano kwenye Katuni tunatakiwa kuzitengeneza zile zenye mahitaji yetu,muhimu kama vyuo vikuu kuyachuja yale yanayokuja teknolojia ipo kila mahali na sawa hatuwezi kuitenga lakini lazima tuwe na sauti kwa manufaa ya jamii,”alisema Dk.Ndossa.

Alisema asilimia kubwa ya watanzania ni wakulima hivyo Vyuo Vikuu vinawajibu wa kuwasaidia ili kuufikia mnyororo wa thamani na kuweza kupata vipato.

Zaidi ya asilimia 60 ni wakulima changamoto ni jinsi ya kuunganisha mnyororo wa thamani vyuo vikuu tuna wajibu na hili,”alisema.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo hicho kutokea Idara ya Geographia, Dk. Fadhili Bwagalilo alisema kuna haja ya kuangalia mbinu za kufundishia kwani wanafunzi wengi wanakuwa mabalozi wa kile ambacho wamefundishwa.

“Wanakuwa ni mabalozi kwani wale aliowakuta kule mpaka wajiliza ametoka chuo gani jibu linakuja moja kwa moja chuo alichotoka hakipo vizuri,” alisema Dk. Bwagalilo.

Naibu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Timoth Simalenga alisema wamejipanga kuhakikisha chuo hicho kinatoa elimu sahihi huku akidai kwamba ushauri waliopewa na Profesa Mwamfupe wameupokea na wataufanyia kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles