24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wanafunzi wenye mahitaji maalum wakosa shule Njombe

Na Elizabeth Kilindi, Ludewa

Wanafunzi wa shule ya maalum ya Mundindi iliyopo kata ya Mundindi Tarafa ya Liganga wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wameshindwa kuendelea na masomo ya Sekondari kutokana na upungufu wa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum mkoani humo.

Hayo yamebainishwa leo Jumamos Desemba 12, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Amos Mtitu baada ya kupokea msaada wa vitu mbalinbali nyenye thamani ya Sh milioni moja na nusu kutoka kwa Mbunge wa Ludewa,Joseph Kamonga aliyetoa kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.

Mtitu amesema wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa wakifaulu elimu ya msingi lakini yanapofanyika machaguo wamekuwa wakipelekwa shule za sekondari za kata ambazo hazina wataalam.

Amesema shule hiyo ina makundi matatu ya wanafunzi wasioona, viziwi na wenye ulemavu wa akili hivyo wanafunzi wanapofaulu wanahitaji walimu ambao wanaweza kuwasiliana nao kwa kwa alama.

“Ukimpeleka mwanafunzi shule ambayo hakuna mwalimu wa alama Wala wa kumuhudumia hivyo akikosa mawasiliano anakata tamaa na kurudi nyumbani,” amesema Mtitu.

Upande wake Mwakilishi wa Mbunge huyo, Stanley Gowele mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo amesema kutokana na kutambua umuhimu wa kundi hilo maalum mbunge Kamonga amemuagiza kufikisha salamu hizo kwa kundi hilo maalum kwenye maeneo machache ya Ludewa ambayo aliona amefanikisha jambo juu yao.

“Tulianza na Kijiji cha Mavanga pale kulikuwa na mlemavu ambaye mbunge alimuona kipindi cha kampeni alikuwa na uhitaji wa msaada wa baiskeli hivyo kwa niaba yake tumemkabidhi baiskeli hiyo yenye thamani ya shilingi laki tano,”amesema Gowele.

Nae, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa ambaye pia diwani wa kata ya Mundindi, Wise Mgina amesema wanafunzi hao wakipewa elimu inayofaa na wakapelekwa katika shule zinazostahili watakuwa na msaada mkubwa kwa jamii.

“Wanafunzi wanafaulu lakini wanapangiwa shule ambazo wakienda wanakutana na walimu ambao siyo wa elimu kada hiyo kuna changamoto kwa sisi wenyewe pengine hatufikishi ujembe kwa watu wakajua kama kuna mazingira Kama hayo,” amesema Mgina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles