Na GLORY MLAY-DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Ihefu, umesema wameanza kuboresha Uwanja wao wa nyumbani wa HighLand Estates, kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu Mkuu wa timu Fredy Chalamila, alisema mechi tatu za mwanzo hazitachezwa kwenye uwanja huo bali wattaumia ule wa Sokoine.
Alisema wanafanya marekebisho katika ujengaji wa kuta, Majukwaa na vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji.
“Tumeshaanza marekebisho ya uwanja huu na mechi tatu za mwanzo hatutautimia kwasababu utakuwa bado haujakamilika, tutatumia uwanja wa Sokoine, marekebisho yanaendelea na matumaini yetu tutaumaliza mapema,” alisema.