27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanaharakati aliyeandamana na Martin Luther afariki

WASHINGTON, MAREKANI

MWANAHARAKATI na shujaa wa haki za binadamu nchini Marekani John Lewis ambaye aliandamana na Martin Luther King Jr, na kukaribia kuuwawa kwa kupigwa na polisi, kabla ya kuhudumu kama mbunge kwa miongo kadhaa, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80. 

Lewis ambaye ni Mmarekani mweusi alitumia maisha yake kutafuta kile alichokiita shida nzuri, kwa kushiriki mikutano muhimu ya kuboresha demokrasia ya Marekani katika kukomesha ubaguzi na ukosefu wa haki za binadamu. 

Lewis alikuwa kijana mdogo wakati wa maandamano ya mwaka 1963 jiijini Washington, ambayo Martin Luther King Jr, alitoa hotuba ya nina ndoto. 

Miaka miwili baadae mwanaharakati huyo alikoswakoswa kuuwawa pale alipokuwa akiwaongoza mamia ya waandamanaji kuvuka daraja la Edmund Pettus huko Selma, Alabama kuelekea Montgomery ambapo askari waliwashambulia waandamanji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles