26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Twitter yadukuliwa

CALIFORNIA, MAREKANI

KAMPUNI ya mtandao wa Twitter imesema wadukuzi walifanikiwa kupakua data katika jumla ya akaunti 8 kwenye uhalifu uliotokea wiki hii.

Pamoja na hayo, twitter imesema kuwa akaunti hizo hazikuwa zimethibitishwa. Mapema wiki hii wadukuzi wasiojulikana walizilenga jumla ya akaunti 130 na kufanikiwa kudhibiti karibu akaunti 45. 

Watu mashuhuri na viongozi waliolengwa ni pamoja na mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden, rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na bilionea Elon Musk. 

Wahalifu hao walitumia sarafu ya mtandaoni ya Bitcoin katika uhalifu huo na zaidi ya dola 100,000 ziliibwa. 

Kwenye taarifa yake Twitter imesema wadukuzi walifanikiwa kufungua taarifa binafsi ikiwemo barua pepe, anuani na namba za simu kwenye akaunti zilizolengwa. 

Shirika la FBI linaongoza uchunguzi katika uhalifu huo uliofanyika Jumatano na wabunge wametaka mtandao huo kuwajibishwa mara moja.

Hii si mara ya kwanza kwa mtandao wa Twitter ambao umezidi kujizolea umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni kudukuliwa.

Mwaka 2017  anuani kadhaa za mtandao wa Twitter, ikiwemo ile ya klabu ya mpira wa miguu nchini Ujerumani, wizara za Ufaransa na ile ya chaneli ya BBC Amerika Kaskazini, zilifanyiwa udukuzi na maharamia wa mtandao.

Maharamia hao walitajwa kama ni wafuasi wa Serikali ya Uturuki walioweka ujumbe wa kukashifu Utawala wa Kinazi wa Ujerumani na ule wa Uholanzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles