Aveline Kitomary
Ni muhimu kwa mjamzito kuanza kuhudhuria kliniki mapema ili kulinda afya yake na mtoto aliye tumboni. Kwa kutambua umuhimu wa kulinda afya ya mama na mtoto, serikali imefanya mapinduzi katika sekta ya afya ikiwa ni ku- jenga miundombinu hasa ujenzi wa vituo vya afya kwa kila kata lengo likiwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.
Serikali na taasisi binafsi zime- kuwa na ushirikiano hasa katika kukabiliana na magonjwa yanay- owasibu wajawazito hususani tatizo la fistula.
Fistula ni aina ya ugonjwa ambao huweka shimo kubwa kati ya njia ya uzazi na njia ya mkojo unatokana na mama kuwa na uchungu wa muda mrefu bila matibabu.
Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji kutoka hospitali ya CCBRT, Dk. James Chapa, tatizo hilo huwaathiri zaidi wasichana ambao wanapata mimba wakiwa na umri mdogo na kujifungua kabla mifupa ya sehemu za kizazi ikiwa bado haijakomaa ipasavyo.
Anasema wanawake ambao tundu la kizazi chao ni dogo au wale ambao wamekeketwa wako katika hatari kubwa ya kupata maradhi hayo.
Anaeleza kuwa wanawake ambao wameathirika na mara- dhi hayo huvuja mkojo mara kwa mara bila kukusuadia, harufu mbaya ya mkojo hufanya waathirika kutengwa na kunyan- yapaliwa kwa kudhaniwa kuwa ni wachafu.
“Mtatizo mengine yanayoto- kana na maradhi hayo ni ukosefu wa maji ya kutosha mwilini na utapiamlo,” anabainisha.
Dk. Chapa anasema ugonjwa wa fistula humdhalilisha mwan- amke na kumsababishia madhara mengine ya kiafya.
“Ili mwanamke apone ugonjwa huu ni vyema akatibiwe hospi- tali kwani hakuna eneo mbadala ambalo tiba inapatikana.
“Matibabu yakifanyika mape- ma na kuwa na ufasaha majibu huwa mazuri kwa zaidi ya asil- imia 90 hivyo, kama yupo mwe- nye tatizo hili na bado hajafika hospitali afike CCBRT kwaajili ya matibabu,” anasema.
TAKWIMU ZILIVYO
Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), za mwaka 2018 zinaonyesha kuna wanawake takribani milioni mbili wanaishi na fistula duniani.
Inakadiriwa kuwa wagonjwa wapya kati ya 50,000 na 100,00 hupatikana kila mwaka, wakati juhudi za kutibu fistula duni- ani huishia kutibu wagonjwa 20,000 tu.
Idadi kubwa ya wagonjwa wenye fistula wapo zaidi barani Afrika hususan kusini mwa Jangwa la Sahara huku nusu wakiwa nchini Nigeria, mabara mengine ni Asia na Amerika ya Kusini.
Hapa nchini, takwimu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto zinakadiria kuwa na wanawake takribani 2,500 ambao hupata fistula kila mwaka, huku idadi ya wanaopatiwa matibabu kila mwaka ikiwa ni takribani wa- nawake 1,000 kwa mwaka.
“Katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2015 hadi De- semba, 2019 wanawake zaidi ya 5,500 walitibiwa fistula.
“Mafanikio haya yanatokana na kampeni iliyoendeshwa kwa ushirikiano baina ya serikali na wadau ambayo imeweka mabalozi wa fistula zaidi ya 3,000 nchi nzima wanaosaidia kuratibu rufaa na usafiri kwa wagonjwa kwenda hospitali zinazotoa huduma ya fistula,” anasema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.
AINA ZA FISTULA
Dk. Chapa anasema zipo fistula ambazo hazisababishwi na masuala ya uzazi.
“Upo ugonjwa wa saratani unaweza kusababisha aina ny- ingine ya fistula, pia matibabu ya mionzi yanaweza kusababi- sha ugonjwa huo.
“Mtu akipata jeraha kuto- kana na ajali yoyote anaweza kupata fistula na magonjwa mengine kama kichocho na kibofu cha mkojo ambayo husababisha fistula,” anasema.
Dk. Chapa anasema upas- uaji nao husababisha fistula na hii huhusisha mirija inapotoa mkojo kwenye figo kupeleka katika kibofu.
“Mirija hii mara nyingi hupita karibu na kizazi na upasuaji huhusisha kizazi, mirija hii ikitokea kukatwa au kufungwa wakati wa upasuaji, pia kibofu cha mkojo kipo ka- ribu na kizazi hivyo wakati wa upasuaji jeraha hutokea eneo la kibofu na kusababisha fistula,” anasema.
INAWEZA KUJIRUDIA
Dk. Chapa anasema mama aliyefanyiwa upasuaji kabla ya kuondoka hospitali ni vyema akamuuliza daktari endapo ku- likuwa na tatizo lolote wakati wa tukio hilo.
“Kuna uwezekano wa kutokea majeraha wakati wa upasuaji hivyo mama anapofa- hamu kama kulikuwa na tatizo akashauriwa nini cha kufanya baada ya kuruhiusiwa.
“Kama kulikuwa na jeraha katika kibofu mama huwekewa mpira wa kutolea mkojo ili apumzishe kibofu cha kutolea mkojo kuanzia siku 10 hadi 14. “Pia mama huyu atashauriwa kunywa maji na kuwa msafi ili kuepusha maambukizi katika viungo vya uzazi,” anasema.
Dk. Chapa anasema mgonjwa aliyetibiwa fistula upo uwezekano wa kuupata ugonjwa huo kwa mara nyingine.
“Tunapowatibu wagonjwa masharti tunayowapa ha- waruhusiwi kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya upas- uaji huo, uzazi utakaofuata ni kwa upasuaji ili kumwepusha mtoto kupita njia ya kawaida na kufumua eneo ambalo lilirekebi- shwa,” anasema.
Dk. Chapa anasema mama anashauriwa baada ya miezi minne ndio hupendekezwa kushiriki mapenzi na ataka- poanza kinyume na muda huo uwezekano wa ugonjwa huo kurudi ni mkubwa.
WANAOATHIRIKA ZAIDI
Dk.Chapa anasema wa- naoathiriwa zaidi na fistula ni ambao hawajafika umri salama kwaajili ya uzazi, kuanzia miaka 18 na kuendelea.
“Mtu akipata mimba kabla ya umri huo uwezekano wa kupata fistula ni mkubwa kwa sababu nyonga yake haijakomaa, pia inawapata kina mama wa umri wowote, ukilinganisha na wenye miaka 18 na kuendelea waliopata ujauzito na wenye umri chini ya hapo wanauwezekano wa kupata fistula mbaya zaidi kwa sababu wanapata majeraha makubwa,” anasema.
UELEWA MDOGO
Dk. Chapa anasema bado uelewa wa jamii juu ya ugonjwa fistula ni mdogo. “Watu hawajui chanzo cha ugonjwa na matib- abu yake nini kwahiyo inaathiri mtiririko wa wagonjwa kuja kupata matibabu.
“Kama mtu haamini hili ni tatizo la kawaida ni ngumu kum- shawishi kutafuta matibabu, pia wanapofika hospitali tunakutana na changamoto za afya zao.
“Mtu anakuja akiwa na upungufu wa damu, magonjwa mengine ambayo hayakutibika vizuri kama presha na kisu- kari ambayo hutupa changamoto kumhudumia mgonjwa vizuri,” anasema.
Changamoto nyingine anayoi- taja Dk. Chapa ni tatizo la kiakili ambalo huwakumba wagonjwa hao.“Wengine wanakuja tayari wana shida ya kiakili kum- saidia inakuwa changamoto, kwa sababu matibabu yetu yanahitaji ushirikiano baina ya wataalamu na mgonjwa mwenyewe.
Baada ya upasuaji mgonjwa anapaswa kuwa katika mashine ya kutolea mkojo kwa siku 14 na anahitajika kunywa maji kila siku.
“Kwahiyo, mtu ambaye akili haikuwa sawa hawezi kufuata masharti baada ya upasuaji hivyo tunajitahidi muda wote kukabiliana nao.
Pia baada ya upasuaji watu hawafuati masharti tunayotoa baada ya upasuaji ndio maana utakuta wengine ugonjwa hu- rudi,” anasema.
UMASKINI NI TATIZO
Furaha Mafuru, ni Ofisa Programu Kitengo cha Mama
na Mtoto Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), anasema tatizo la fis- tula huwapata wanawake wengi wasio na kipato cha kutosha, hali ambayo huwasababisha kwenda kujifungulia kwa wakunga wa jadi au nyumbani.
“Kwa sababu hawana uwezo inakuwa ni changamoto kwao ku- toka nyumbani kwenda hospitali kwaajili ya matibabu, hii huwa chanzo cha wao kupata ugonjwa huu kutokana na kuchelewa mat- ibabu,” anasema.
Anasema katika kuimarisha huduma za haraka za kujifungua, serikali ikishirikiana na wadau uboreshaji mkubwa wa vituo vya kutoa huduma haraka ume- fanyika.
“UNFPA ikishirikiana na serikali imeboresha vituo katika Mkoa wa Simiyu Kigoma katika kipindi cha miaka miwili, tume- karabati vituo vya afya 40 Simiyu na vituo sita Kigoma na sasa kina mama walio mikoa ya pembezoni kwasasa hawapati shida kwa sababu vituo vilivyoboreshwa vimewekwa vifaa na kina mama wanapatiwa mafunzo ya kukabili- ana na hatari yoyote wakati wa kujifungua,” anasema.
HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI
Kutokana na kuimarishwa kwa huduma, Waziri Ummy anasema idadi ya wanawake wanaojitokeza kutibiwa fis- tula katika hospitali za CCBRT, Bugando, Nkinga na Kuvulini Maternity Center, imepungua kwa zaidi ya asilimia 30.
“2016 walikuwa wagonjwa 1356; mwaka 2017 idadi hiyo ikashuka na kufikia 1060, mwa- ka 2018 ikashuka tena na kufikia idadi ya wanawake 900, na 2019 ikashuka zaidi na kufikia wa- nawake 852.
“Hii imetokana na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za upasuaji wa dharura chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magu- fuli,” anasema.
Ummy anasema serikali imei- marisha huduma kwa wajawa- zito, hatua ambayo imesaidia kupunguza matatizo ya fistula kwa wanawake wengi nchini.
“Wajawazito waliotimiza mahudhurio manne au zaidi (ANC4+) mwaka 2019/20 wali- fikia asilimia 77 ikilinganishwa na asilimia 41 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/2016.
“Kina mama wanaojifun-
gulia vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 83 Machi mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 64 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/16. “Idadi ya vituo vya afya vinavyotoa huduma ya dharura kwa wajawazito (CEMONC) im- eongezeka na kufikia vituo 352; Machi mwaka 2020 ikilingan- ishwa na vituo 115 mwaka 2015,” anasema.