MANCHESTER ,ENGLAND
CHAMA cha Soka England (FA) kimeahirisha mechi ya Ligi Kuu kati ya Manchester City na Arsenal uliotakiwa kuchezwa jana katika Uwanja wa Etihad jijini Manchester ikiwa ni hatua ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.
Hatua hiyo ilifikiwa baada ya baadhi ya wachezaji wa Arsenal walikaribiana na mmiliki wa klabu ya ya Olympiacos, Evangelos Marinakis ambaye juzi ilitoka taarifa kuwa ameambukizwa virusi vya COVID-19 vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Corona.
Bosi huyo
alikuwepo katika Uwanja wa Emirates February 27, mwaka huuwakati timu yake
ilipocheza na Arsenal katika michuano ya Europa na uchunguzi umeonesha kuwa
alikaribiana na wachezaji wa Arsenal pamoja na baadhi ya wafanyakazi hivyo
hatua stahili imebidi zichukuliwe.
Agizo la
serikali ya Uingereza kuwa mtu yeyote atakayethibitika kukaribiana na mtu
aliyeambukizwa kirusi hicho anapaswa kutengwa nyumbani kwa siku 14, hivyo
Arsenal imeagiza wachezaji wao pamoja na wafanyakazi na viongozi waliokaa nae
karibu wakati wa mchezo wasalie majumbani mwao kwa leo na kesho ili kukamilisha
siku 14.
Hali hiyo imepelekea mchezo wa kiporo ambao
ulikua kuhairishwa tena hadi utakapopangwa siku nyingine.
Evangelos Marinakis ambaye pia ni Mmiliki wa Klabu ya Nottingham Forest ametangaza kupata Corona ikiwa ni siku chache baada ya kuhudhuria mchezo wa Nottingham dhidi ya Millwall.
Hata hivyo,
Arsenal imesema hatari ya wachezaji hao kupata maambukizi ni ndogo kwa mujibu
wa wataalamu wa afya, lakini wanafuata taratibu zilizowekwa na serikali ili
kudhibiti maambukizi kusambaa zaidi
Iwapo wachezaji wa Arsenal watathibitika kuwa
salama, watarejea mazoezini siku ya Ijumaa kujiandaa na mchezo dhidi Brighton
& Hoves Albion.
Ugonjwa wa Corona ulilipuka Wuhan nchini China Disemba mwaka jana na kusambaa nchi mbalimbali ambapo sasa unaripotiiwa kufika katika nchi zaidi ya 85 duniani.
Italia ndiyo nchi inayoongoza kwa kesi za Corona Barani Ulaya, ambapo hadi sasa watu 400 wameripotwa kuambikizwa virusi hivyo vinavyosambaa kwa njia mbalimbali ikiwemo ya hewa.