25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

SamaKiba yazindua jezi zake Dar

BRIGHTER MASAKI – Dar es Salaam

TAASISI ya SamaKiba inayouundwa na staa wa soka nchini Mbwana Samatta na Ali Kiba, imezindua jezi zake mpya zitakazotumika katika msimu mwingine wa kampeni ya Nifuate.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kiba alisema baada ya kutangaza tenda ya kuandaa jezi hizo, mfanyabiashara wa mavazi,  Fred Vunja Bei alishinda na mwaka huu zitapatikana nchi nzima.

“Tuliona uhitaji wa jezi tukaamua tutangaze tenda, yakaja makampuni saba na Fred Vunja Bei akawa ameshinda, kwahiyo msimu huu jezi zitakuwa zinapatikana zikiwa na viwango na ubora mkubwa,” alisema Kiba.

Aidha alisema sababu za kuwa kimya kwenye muziki ni utaratibu wake wa kuachia wimbo na kutoa nafasi kwa mashabiki kuufurahia japo wafuasi wake wanataka atoa nyimbo mara kwa mara.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles