29.9 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Kamati ya Nahodha yakosa theluthi mbili

Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha
Mwenyekiti wa Kamati namba moja ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha

Na Debora Sanja, Dodoma

MWENYEKITI wa Kamati namba moja ya Bunge Maalumu la Katiba, Shamsi Vuai Nahodha, imekosa theluthi mbili katika ibara mbili wakati wakipitisha sura ya pili na ya tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana alisema kamati yake imeshamaliza kujadili sura ya pili na sura ya tatu pamoja na kupitisha ibara za sura hizo kwa kupiga kura.

Kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba, sura ya kwanza inahusu malengo muhimu, misingi ya mwelekeo wa shughuli za Serikali na sera za kitaifa.

Sura ya tatu inahusu mamlaka ya wananchi, utii na uhifadhi wa Katiba ambayo ina sehemu mbili za maadili na miiko ya uongozi wa umma.

Alisema wakati wa kupiga kura ibara ya 19 ilikosa theluthi mbili kwa upande wa Zanzibar na Ibara ya 21 ilikosa theluthi mbili kwa upande wa Tanzania Bara.

“Ibara ya 19 inahusu kiongozi au mtu yeyote yule kutoruhusiwa kutumia mali ya umma, wakati ibara ya 21 inamtaka mtumishi wa umma aliye katika ajira ya kudumu kutoruhusiwa kuingia katika ajira nyingine yoyote yenye malipo ya mshahara pamoja na kutoruhusiwa kuchaguliwa au kuteuliwa kushika madaraka katika chama cha siasa,” alisema.

Alisema pamoja na wajumbe wa kamati hiyo kujadili sura hizo, wamefanya marekebisho ya kimaudhui kidogo  pamoja na mabadiliko ya lugha.

Alitoa mfano kipengele cha rasimu kinachomtaka mtumishi wa umma atakayeiba afukuzwe kazi badala yake kamati imefanya marekebisho kwa kutaka mtumishi huyo achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria za nchi.

- Advertisement -

Related Articles

2 COMMENTS

  1. lait kama serekali ingewaelimisha wananchi mapema kujua katiba yao ya zamani na kujua mapungufu na mazuri yaliyomo kwenye katiba hususan mfumo wa serekali haya yote yasingetokea. najua viongoz walioko madarakani hawakusoma alama za nyakati na haya ndo matokeo yake.najua jua litoke lisitoke lazima katiba ikamilike kwa namna ccm walivyojipanga kutaka maoni yao ndo yapite, lakini kamwe haitakuwa katiba bora na itakayo dumu kwa muda mrefu.nashauri jamii iendelee kuelimishwa ili kuujua ukweli kwan najua baada ya kumaliza mchakato hu watarudi kw wananchi kuwahadaa kwa maneno mazuri na kwa vile watanzania wengi wanaishi vijijini na wala hawafuatilii mchakato huu na kwa vile wabunge wengi wa ccm wamepata ubunge maeneo ya vijijini mahali ambapo wananchi wengi wanaamini baba wa taifa bado yupo hai na hakuna chama kingine zaidi ya ccm ni rahisi tu kuwadanganya.Tahadhari kwa ccm wakiona kuwa wao ndo wako sahihi zaid na kuendelea kubeza maoni ya wananchi wajue wanajichimbia kaburi wenyewe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles