27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

JK atoa somo la maendeleo Afrika

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete

NA MWANDISHI MAALUMU, WASHINGTON

RAIS Jakaya Kikwete amesema sababu kubwa inayokwamisha maendeleo ya haraka kwa Afrika ni uzalishaji pamoja na matumizi madogo ya umeme.

Alisema hayo juzi kwenye mkutano wa kwanza wa wakuu wa nchi za Bara la Afrika uliofanyika chini ya uenyekiti wa Rais wa Marekani, Barack Obama, ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo.

Rais Kikwete alisema bila kuwapo ongezeko kubwa la uzalishaji na matumizi ya umeme, Bara la Afrika halitatoka kwenye uduni.

“Kwa mujibu wa ripoti ya Kanda ya Shirika la Umoja wa Mataifa Mazingira (UNEP), matumizi ya umeme katika Afrika ni asilimia 31 tu na hivyo kulifanya bara hilo kutumia asilimia tatu tu ya umeme wote duniani.

“Uelewa mdogo wa matumizi ya umeme ya Bara la Afrika ni kuangalia matumizi ya nishati hiyo kwa kila mkazi wa bara hilo na yule wa Marekani. Wakati kila raia wa Marekani anatumia kilowati 13,246, katika Afrika, wastani ni kilowati 440,” alisema Rais Kikwete.

Alisema ukiondoa nchi ya Afrika Kusini, matumizi ya umeme kwa kila raia wa Afrika yanateremka na kufikia kilowati 160.

“Uzalishaji wa jumla wa umeme wa Bara la Afrika ni megawati 63, ambazo ni sawa na umeme unaozalishwa na nchi moja tu ya Ulaya ambayo ni Hispania,” alisema.

Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku tisa nchini Marekani, na leo ataondoka jijini Washington D.C kwenda Houston ambako atafungua na kushiriki mkutano wa uwekezaji na uchumi Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles