26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti h’mashauri Igunga, mwenzake kortini kwa uvamizi wa shamba

Abdallah Amiri, Igunga.

DIWANI Kata ya Choma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Peter  Maloda (CCM) na Ndekwamima Usukani, wamefikishwa Mahakama ya Mwanzo Choma kwa tuhuma ya kuvamia shamba la Tungu Ntengwa.

Awali akiwasomea mashtaka washtakiwa wote kwa pamoja mwishoni mwa wiki iliyopita, Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Choma, Simon  Malima alidai wote wanakabilwai   na kesi namba  65/2019.

Alisema Desemba 16, mwaka huu, saa 3 asubuhi katika Kijiji cha Choma, washitakiwa wote kwa pamoja walikutwa wakilima shamba la ndugu Ntengwa mkazi wa kijiji hicho.

Alisema washtakiwa wote walitenda kosa hilo kinyume na kifungu 299  sura ya 16 A kanuni ya adhabu iliyofanyiwa mapitio 2002 inayozuia kufanya makosa kama hayo.

Baada ya hakimu Malima kuwasomea shitaka, washitakiwa wote kwa pamoja walikana kutenda kosa hilo hata  kabla ya kuahirisha kesi hiyo, Malima alisema yeye ameamua kujitoa kusikiliza kesi hiyo.

Alisema sababu iliyomfanya kujitoa katika kesi, ni kwa sababu mtuhumiwa mmoja ni jirani yake anaweza kushindwa kutenda haki katika uamuzi.

Alisema tayari amemuomba Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Igunga, kupeleka hakimu mwingine kusikiliza kesi hiyo.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Januari 7, mwakani, itakapoanza kusikilizwa na hakimu mwingine atakayepangwa ambapo washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana ya Sh 500,000 kila mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles