WASHINGTON, MAREKANI
MAHAKAMA nchini Marekani imeanzisha uchunguzi wa uhalifu juu ya ule wa awali wa Mueller.
Msingi wa hatua hiyo ni sakata la tuhuma za Rais Donald Trump kudaiwa kusuka mpango na Urusi ili kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2016.
Hatua ya uchunguzi wa awali kugeuzwa na kuwa uchunguzi wa jinai inamaanisha kwamba wachunguzi wanaweza kuagiza watu wafike mahakamani kutoa ushahidi na kutolewa kwa nyaraka kwa ajili ya kesi hiyo.
Rais Trump kwa muda mrefu amekuwa akidai ripoti za uchunguzi za Robert Mueller za kula njama na Urusi ni za ‘hila’
Uchunguzi kuhusu Urusi haukubaini kuwepo kwa njama zozote za kiuhalifu baina ya utawala wa nchi hiyo na kampeni za Trump.
Hata hivyo hatua hiyo haikumwondolea Trump kosa la kukwamisha sheria kuchukua mkondo wake.
Ripoti juu ya uchunguzi wa uhalifu kwa mara ya kwanza ulichapishwa katika gazeti la New York Times.
Haijawa wazi juu ya uhalifu unaoweza kujitokeza chini ya uchunguzi huo, lilisema gazeti hilo.
Tathmini ya kiutawala kuhusu uchunguzi uliofanywa na Mueller ulianza mwezi Mei.
Tathmini hiyo inasimamiwa na Mwanasheria Mkuu wa Marekani, William Barr na kuendeshwa na Mwendesha-Mashtaka Mkuu wa Marekani, John Durham.
Durha alipewa jukumu la kubaini ikiwa ukusanyaji wa taarifa za kijasusi kuhusu kampeni ya mwaka 2016 ya Trump ilikuwa ni ya kisheria.
Uchunguzi wa Robert Mueller umechukua takribani miaka miwili.
Mwezi Aprili mwaka huu , Barr aliwaambia wajumbe wa baraza la Congress kwamba anaamini “upelelezi ulifanyika ” juu ya kampeni ya Trump mwaka 2016, akiongeza kuwa: “Swali ni ikiwa ulipangwa vya kutosha . Na sisemi kwamba haukupangwa vya kutosha . Lakini ninahitaji kuchunguza hilo .”
Wakosoaji wanamtuhumu Barr kuanzisha tathmini ya kiutawala hasa zaidi kwa malengo ya kumtafuta rais kuliko kwa ajili ya maslahi ya kisheria.
Katika taarifa ya pamoja , wenyekiti wa mahakama na kamati za ujasusi walisema taarifa za uchunguzi wa uhalifu “ziliibua hofu mpya kwamba idara ya mahakama chini ya Mwanasheria Mkuu Barr imepoteza uhuru wake na inatumika kama chombo cha kulipiza kisasi kisiasa dhidi ya rais Trump “.
Wabunge wa Democrats, Jerry Nadler na Adam Schiff, amesema kuwa hatua hiyo inaweza kuleta “matatizo mapya ambayo hayawezi kusahihishwa ” kwa utawala wa sheria.
Hadi sasa, idara ya mahakama, haijaweka wazi ni uhalifu gani unachunguzwa.
Pia haijawa wazi ni kwanini uchunguzi huu umeanza sasa, au umesababishwa na nini.
Na kwa kuwa idara yenyewe ya mahakama ndiyo iliyomchagua Robert Mueller kuchunguza najam hizo za Urusi katika uchaguzi wa mwaka 2016, uchunguzi huu wa uhalifu unamaanisha kuwa idara hiyo inaweza kuwa inajichunguza yenyewe.
RIPOTI YA MUELLER
Ripoti ya Muller ya kurasa 448- haijasema kama kulikuwa na njama za uhali kati ya Urusi na Trump
Hata hivyo ilielezea mifano 10 ambapo kulikuwa na uwezekano wa Trump kujaribu kuvuruga uchunguzi.
Ripoti hiyo ilisema kwamba Urusi iliingilia katika uchaguzi kwa mtindo wa “uliopangwa na haraka”.
Uingiliaji huo ulifanyika kwa mtindo wa kampeni ya kando iliyopitia mitandao ya kijamii na udukuzi wa faili za kompyuta za chama cha Democrat uliofanywa na idara ya ujasusi ya jeshi la Urusi.