25.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Brigedia Mkeremy aishauri TFS

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy amesema taasisi hiyo inafanya kazi kubwa kuhakikisha inasimamia rasilimali za misitu zilizopo ili ziwe endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Brigedia Jenerali Mkeremy ameyasema hayo akiwa kwenye Msitu wa Hifadhi ya Mazingira asili ya Kalambo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kutembelea maeneo ya hifadhi za misitu na mashamba ya miti ya serikali.

Amesema uamuzi wa serikali kuupandisha hadhi msitu wa Kalambo kuwa msitu wa hifadhi ya mazingira asili ni jitihada za kuhakikisha maporomoko ya mto huo yanahifadhiwa na kusimamiwa ipasavyo.

Amesema ni wakati sasa kwa Watanzania kuanza kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi hiyo ili kujionea maajabu ya maporomoko hayo.

“Eneo hili linavutia na zuri kwa utalii, nitowe wito kwa Watanzania wakiwa katika siku za mapumziko na sikukuu kutembelea na kushuhudia maajabu ya maporomoko haya ambayo yameshatangazwa na Shirika la Umoja wa Matifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni (Unesco) kuwa ni urithi wa dunia.

“Niwapongeze TFS kwa ujenzi wa ngazi zenye urefu wa mita 1,277 zinazoshuka hadi kwenye maporomoko haya yanayomwaga maji ziwa Tanganyika. Nimeambiwa kuwa katika ngazi za kushuka chini kwenye maji kuna sehemu kuu tatu, ya kwanza unapotoka kwenye maji imepewa jina la Waziri wa Maliasili na Utalii, “Kigwangala view point” napendekeza katika “view point” ya pili ambayo ni ya kwanza unapoteremka ngazi iitwe Dos Santos View point na ya tatu inayofuatia iitwe, “Mkeremy view point,” amesema.

Kwa upande wake Kamishna Mhifadhi wa Misitu, Profesa Dos Santos Silayo amesema TFS imeweka mikakati kadhaa katika kuhakikisha misitu yake inaingiza mapato ya kutosha kupitia huduma za utalii sambamba na kuuza mazao ya misitu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles