22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Aliyejifanya Askari amepandishwa kizimbani

Erick Mugisha, Dar es salaam

MKAZI wa Tabata Segerea David Ramadhani (33) aliyejifanya Askari wa Jeshi la Wananchi amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es salaam kwa makosa mawili likiwemo kukutwa na vifaa vya Umma.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Joyce Moshi na Mwendesha Mashtaka wa Serikali ASP Hamisi alidai julai 19, 2019 eneo la  Makao Makuu JKT Mlalakua wilayani Kinondoni Dar es salaam kwa nia ya udanganyifu alijitambulisha kuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi kwa cheo cha MP.

Katika shtaka la pili julai 19, 2019 eneo la Makao Makuu ya JKT Mlalakua wilayani Kinondoni Dar es salaam alikutwa na vifaa vya Umma kinyume na sheria kama sare kamili za askari, sare za askari za kijani, beji na vyombo vya askari, kofia ya askari, kofia ya askari wa usalama wa barabarani, sare za viatu za askari , buti, pingu na redio call.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka mbele ya Mahakama na ASP Hamisi alisema upelelezi wa shauri hili unaendelea tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Hakimu Moshi alisema dhamana yake ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye kusaini bondi ya sh 2,000,000 kila mmoja, barua za utambulisho na nakala ya vitambulisho.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi kesi yake itakapo kuja kusomwa tena septemba 2 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles