33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 20 wauawa nchini Marekani

TEXAS-Marekani

KARIBU  watu 20 wameuawa, huku wengine 26 wakijeruhiwa wakati wa  ufyatuliaji wa risasi katika duka la jumla mjini El Paso, jimboni Texas Gavana wa jimbo hilo, Greg Abbot alilitaja shambulio hilo kuwa mojawapo ya siku mbaya zaidi katika historia ya jimbo  hilo.

Maofisa wa polisi, wanachunguza iwapo shambulio hilo ambalo lilifanyika maili chache kutoka kwa mpaka wa Marekani na Mexico, lilikuwa la uhalifu wa chuki.

Mtu mwenye umri wa miaka 21, sasa anazuiliwa na maofisa wa polisi.

Polisi wanasema, mshukiwa  alikuwa akiishi katika eneo la Allen , Dalla umbali wa  kilomita 1,046 mashariki mwa El Paso. Ametajwa na vyombo vya habari vya Marekani kuwa, ni Patrick Crusius.

Kanda za video za CCTV zilizodaiwa kuwa za mshambuliaji huyo ambazo zilionyeshwa katika vyombo vya habari vya Marekani, zinaonyesha mtu aliyekuwa amevalia fulana  nyeusi na vilinda masikio.

Shambulio hilo, linaaminika kuwa la nane katika historia ya sasa nchini hapa.

Linatokea chini ya 24, baada ya shambulio jingine la kuwafyatulia risasi watu waliokongamana, mjini Dayton Ohio na chini ya wiki moja, baada ya mshambuliaji kijana kuwaua watu watatu katika tamasha la chakula mjini California.

Maofisa wa polisi na wenzao wa ujasusi wa Shirika la Upelelezi (FBI), wanafanya uchunguzi iwapo manifesto ya kitaifa iliochapishwa katika kundi moja la mtandao, iliandikwa na mshambuliaji huyo.

Chapisho hilo, linadai shambulio lililenga jamii ya Wahispania.

Duka hilo ambalo liko karibu na duka jingine kubwa kwa jina Cielo Vista Mall, lilikuwa limejaa wateja waliokuwa wakinunua bidhaa za wanao wao kurudi shule.

Rais wa Marekani, Donald Trump alielezea shambulio hilo kama kitendo cha uoga.

”Najua tunaungana na kila mtu katika taifa hili kushutumu kitendo hiki cha chuki, hakuna sababu ambazo zinaweza kukufanya kuwaua watu wasio na hatia” , alindika katika mtandao wake wa Twitter.

Waathirika bado hawajatajwa, lakini Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador alisema raia wake watatu, ni miongoni mwa waliofariki dunia, kulingana na Shirika la Habari la Reuters.

“Sisi kama taifa tunaungana kuwaunga mkono waathiriwa na familia zao” , alisema Abbot.

Ofisa Mkuu wa Polisi wa El Paso, Greg Allen alisema ripoti za mtu aliyekuwa akiwafyatulia watu risasi kiholela ndani ya duka hilo, ziliripotiwa mwendo wa saa za Marekani 10:39 na maofisa walitumwa katika eneo la mkasa huo chini ya dakika sita.

Kianna Long, alisema alikuwa katika duka hiyo na mumewe wakati waliposikia mlio wa risasi.

”Watu walikuwa na wasiwasi na kukimbia , wakisema  kulikuwa na mtu aliyekuwa akiwafyatulia risasi, Long aliamba Reuters. Shahidi mwengine,Gleondon Oakley aliambia CNN alikuwa katika duka la bidhaa za michezo karibu na duka la jumla lililopo karibu wakati mtoto mdogo alipotoroka na kuingia ndani na kutuambia kuna mtu anafyatua risasi kiholela katika Walmart.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles