27.4 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Obiang atimiza miaka 40 madarakani

MALABO- Equatorial Guinea

RAIS wa Equatorial Guinea ,Teodoro Obiang Nguema juzi, amesherehekea miaka 40 madarakani na kuwa kiongozi wa Afrika aliyepo madarakani kwa mda mrefu zaidi zaidi.

Obiang Nguema, alichukuwa hatamu ya uongozi wa nchi hiyo kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1979.

Lakini makundi ya kutetea haki za binadamu, yamemtaja Obiang Nguema  mwenye umri wa miaka 77, kuwa kiongozi katili, fisadi na wa kiimla zaidi barani Afrika.

Katika uchaguzi wa mwaka 2016, alishinda uchaguzi wa urais kwa  asilimia 90, kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi.

Sherehe yake ya kuadhimisha miaka 40 madarakani zinafanyika katika miji mitatu mikuu, ikiwa ni pamoja na mji wa kiuchumi wa Bata,Mongomo, nyumbani kwao na Djibloho mji mpya uliyojengwa katikati ya msitu kutokana na fedha za mauzo ya mafuta.

Shirika Amnesty International, mwezi uliyopita lilitoa wito kwa Serikali ya Obiang Nguema kuchukua hatua za “kuheshimu, kulinda, na kudumisha haki za binadamu kote nchini humo”.

Lakini wakosoaji wanasema hakuna ishara kuwa Equatorial Guinea, itazingatia wito huo.

Itakumbukwa aliponea chupuchupu mapinduzi kadhaa ya kijeshi, amekuwa akikabiliana vikali na wapinzani wake na wale waliowahi kupanga njama ya kumg’oa madarakani.

Desemba, 2017, Serikali iliripoti madai ya kutibua jaribio la mapinduzi lililopangwa na wapinzani wake, waliotorokea mataifa ya kigeni.

Juni, mwaka huu, watu 130 waliohusika na jaribio hilo, walihukumiwa kifungo cha miaka 96 jela.

Chama kikuu cha upinzani, Citizens for Innovation (CI), kilipigwa marufuku na mamlaka kuendesha shughuli zake mwaka jana.

Wanachama 21, ikiwamo mbunge pekee wa chama hicho walihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kusababisha “vurugu na kushambulia maofisa wa serikali”.

Katika siku za karibuni, Obiang Nguema anaaminiwa kumuandaa mwanawe wa kiume, Teodorin, kumrithi atakapoachia urais wa nchi hiyo.

Teodorin alipandishwa cheo na kuwa makamu wa rais mwaka 2016 na pia anasimamia idara ya ulinzi na usalama.

Alituhumiwa kwa kutumia zaidi ya mara 1,000 mshahara wake rasmi kujenga jumba la kifahari katika mji mkuu wa Ufaransa pamoja na magari ya kifahari miongoni mwa mali zingine za thamani .

Pia alipigwa faini ya Euro milioni 30 sawa na (Dola milioni 33.5) na mahakama hiyo.

Mwaka 2019, waendesha mashtaka wa Uswisi walimuondolea Teodorin, mashtaka ya uhalifu wa kiuchumi, lakini walizuilia magari yake 25 ya kifahari kama dhamana ya kesi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles