Na GLORY MLAY
MSANII wa Bongo Fleva, Pancras Charlz, maarufu PNC, amsema wasanii wanaotoa nyimbo kila mara wanasababisha soko la muziki hapa nchini kupoteza muelekeo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, PNC alisema, msanii ambaye anajitambua na kujua nini anafanya anatakiwa kuachia wimbo mmoja kwa mwaka au miezi sita ili kuupa nafasi ya kusikilizwa na mashabiki.
“Soko linakufa maana wasanii kwa sasa kama wanashindana, kila mwezi anatoa ngoma, msanii unatakiwa unakaa mwaka mmoja ndio unaachia nyingine ili wimbo huo uishi kwa mashabiki, lakini kutoa kila mara kuna sababisha kupoteza maana ya bongo fleva.
“Wakati mwingine nyimbo hizo hazina ubora wowote ili mradi na yeye anaonekane kwenye Tv au watu wamsikie mtaana lakini hajui kwamba muziki unakufa, tungo zao hazina ubora wanarudia maneno yale yale na nirahisi kupotea masikio mwa watu maana hatojua asikile upi aache upi,” alisema msanii huyo.