Na GLORY MLAY
MWIMBAJI nyota wa Singeli nchini, Aman Khamis ‘Man Fongo’, amesema sababu ambayo ilifanya muziki huo uchelewe kupata mafanikio kwenye soko ni dhana ya uhuni iliotawala tasnia hiyo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Man Fongo alisema muziki huo ulikuwa umeaminika kuwa ni wa kihuni kutokana na tungo zake, uchezaji wake hata ubora wa studio walizokuwa wanatumia kurekodi.
“Muziki huu bado ni mchanga na watu bado walikuwa hawajaupokea, unakuta watu wanacheza na siraha, watu wanaibiana lakini sasa hivi kina mama, watoto, masela na kila mtu anacheza mpaka tunaingia studio kubwa kurekodi,”, alisema Man Fongo.