33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Wenger kuwanoa Iniesta, David Villa

KOBE, JAPAN

ALIYEKUWA kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameripotiwa kuwa yupo kwenye hatua za mwisho kwenda kuifundisha klabu ya Vissel Kobe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan.

Kocha huyo ambaye yupo nje ya uwanja tangu alipofukuzwa katika klabu ya Arsenal mwaka jana baada ya kuitumikia kwa miaka 22, amedaiwa kupewa ofa na klabu hiyo ambayo ndani yake kuna mastaa wa zamani wa Barcelona, Andres Iniesta na David Villa.

Wenger mwenye umri wa miaka 69, baada ya kufukuzwa ndani ya klabu ya Arsenal, nafasi yake ikachukuliwa na Unai Emery na kuifanya klabu hiyo imalize nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu msimu huu.

Endapo mpango huo utakamilika kwa kocha huyo kujiunga na timu hiyo ya nchini Japan, basi itakuwa si mara yake ya kwanza kufundisha soka nchini humo, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1995 alipokuwa anaifundisha klabu ya Nagoya Grampus Eight, ambapo alikaa msimu mmoja kabla ya kwenda kujiunga na Arsenal nchini Uingereza.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Wenger amefikia makubaliano na uongozi wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, ambapo utakuja kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2021.

Hata hivyo, mkataba huo unadaiwa kuwa na thamani ya pauni milioni 3.5 kwa mwaka ambazo atakuwa anachukua kocha huyo raia wa nchini Ufaransa.

Mara baada ya kufukuzwa katika klabu ya Arsenal, Wenger aliweka wazi kuwa bado muda wake wa kustaafu kufundisha soka, atahakikisha anarudi viwanjani mapema iwezekanavyo au baada ya kupumzika kwa muda kidogo.

Lakini kutokana na umri wake, hii inaweza kuwa ni nafasi yake ya mwisho kurudi viwanjani, baada ya hapo atatangaza kustaafu soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles