Elizabeth Joachim, Dar es Salaam
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, amesema Sheria ya Vyama vya Siasa haijaweka sharti kwa mwanachama wa chama cha siasa akihama chama ni lazima akae miaka miwili ndipo agombee katika uchaguzi unaohusisha vyama vya siasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Aprili 5, na Jaji Mutungi, sheria hiyo na kanuni zake haina kifungu kinachoweka masharti kwa mwanachama kuhama kutoka chama kimoja kwenda kingine.
“Hivyo, nawaomba wananchi na wadau wote wakuu kupuuzia habari za uongo na ninawaasa wanaosambaza habari hizo kuacha mara moja kwani wanapotosha wananchi,” amesema Msajili amesema.