21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

TFDA yatoa taulo za kike kwa wanafunzi kidato cha sita walioko kambi ya kitaaluma

Derick Milton, Simiyu

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), imetoa katoni zaidi ya 100 za taulo za kike kwa wanafunzi wa kike 538 wa kidato cha sita walioko kwenye kambi ya kitaaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Akikabidhi taulo hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka, Meneja wa mamlaka hiyo Kanda ya Mashariki Nuru Mwasulama amesema taulo hizo zina thamani ya Sh milioni tano.

“Katika kuunga mkono juhudi za mkoa kuinua elimu, TFDA imeona isaidie sehemu moja wapo kwa wasichana wa kike ambao tunajua kuwa wamekuwa wakipata shida kwenye suala hili hasa wanapoingia kwenye siku zao,” amesema Mwasulama.

Akipokea msaada huo, Mtaka alipongeza TFDA huku akiwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na serikali kuhakikisha inatatua changamoto zote zinazowakabili kwenye kambi hiyo.

Nao baadhi ya wanafunzi wameshukuru msaada huo, kwa kile walichosema kuwa umekuja kwa wakati muafaka ambao wamekuwa wakipata shida kupata taulo hizo wanpoingia hedhi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles