25.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 23, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kigoda azikwa

MTZ DAILY.inddAMINA OMARI, HANDENI NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, umezikwa katika Kata ya Chanika iliyopo Handeni mkoani Tanga.

Mazishi hayo yaliyofanyika jana yaliongozwa na Rais Jakaya Kikwete.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wabunge wakati wa mazishi hayo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema Serikali imepoteza mtu mchapakazi, muadilifu na mwenye fikra za maendeleo ya mageuzi ya uchumi wa nchi hii.

Alisema Dk. Kigoda alikuwa ni msomi aliyetumia taaluma yake katika kushauri na kutetea masilahi mbalimbali ya taifa ili kujiletea maendeleo endelevu.

Makinda alisema jambo ambalo hawatalisahau ni kusaidia kuleta mageuzi ya kimfumo ndani ya Bunge hilo na kusaidia kuleta maendeleo makubwa.

“Tutaendelea kumkumbuka na kumuenzi kutokana na michango mbalimbali aliyoitoa na ushauri katika uendeshaji wa Bunge, hususani katika Kamati ya Fedha na Uchumi aliyowahi kuiongoza,” alisema Makinda.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Serikali, alisema Dk. Kigoda atakumbukwa kwa kuwezesha kusimamia kwa vitendo mikakati ya kuendeleza biashara nchini.

Alisema aliweza kusimamia kwa ukaribu sera ya kuifanya nchi iweze kujiendesha kupitia viwanda vikubwa, vya kati na vidogo katika kupiga hatua za kimaendeleo kwa haraka.

Mwakilishi wa wabunge wa mkoani Tanga, Brigedia mstaafu, Hassan Ngwilizi, alisema wamepoteza kiongozi aliyekuwa shujaa kwa mkoa huo na taifa kwa ujumla.

“Marehemu alikuwa ni mwenyekiti wa wabunge wa mkoa huu, kila mara alikuwa anatushauri na kutuasa ili kuhakikisha tunaleta maendeleo kwa Serikali na wananchi wa mkoa huu,” alisema Ngwilizi.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya vyama vya upinzani, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Zanzibar, Salum Mwalimu, alisema kuwa marehemu amewaachia jambo moja kuwa siasa si ugomvi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles