NA CHRISTINA GAULUHANGA, DAR ES SALAAM
ALIYEWAHI kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Balozi Juma Mwapachu, amerejesha rasmi kadi za Chama cha Tanu na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kadi hizo alizirudisha katika ofisi za chama hicho zilizopo eneo la Mikocheni A jijini Dar es Salaam jana na kuzikabidhi kwa Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Kata ya Mikocheni, Sudi Odemba.
Mwapachu ambaye ni kada mkongwe wa chama hicho, alisema kadi ya Tanu yenye namba 819820 aliipata Aprili 6, 1976 na ya CCM yenye namba 132392 ambayo ni ya zamani, aliipata Mei 19, 1977 na mpya yenye namba 734620 aliipata Novemba 28, 2004 na kuilipia ada mwaka 2015 hadi 2022.
Kwa upande wake, Odemba, alisema amepokea kadi hizo kutoka kwa Mwapachu ambaye alikuwa ni mwanachama ndani ya kata hiyo na ameamua kujiondoa ndani ya chama hicho.