27.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Upinzani wafungua kesi kupinga muswada wa vyama vya siasa

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Vyama 10 vya upinzani nchini vimefungua kesi kupinga muswada wa vyama vya siasa ili ujadiliwe kabla ya kupitishwa kuwa sheria itakayozuia vyama hivyo visifanye mikutano ya hadhara.

Muswada wa sheria ya vyama vya siasa ulipelekwa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa serikali Novemba mwaka jana.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mbele ya wenzie waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Alhamis Januari 3, Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe amesema katika kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu ya kanda ya Dar es salaam, vyama hivyo vinapinga kuwasilishwa kwa muswada huo bungeni ili ujadiliwe maudhui yake na kamati husika.

Amesema kesi hiyo ilifunguliwa Desemba 20 mwaka jana na itaanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza kesho Ijumaa Januari 4, na imefunguliwa na yeye Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Naibu Katibu Mkuu Bara Chama cha Wananchi (CUF) Joram Bashange na Mkurugenzi wa habari, Uenezi na mawasiliano ya umma wa chama hicho Salim Abdalla Bimani kwa niaba ya vyama hivyo.

“Tumeamua kupeleka suala hili mahakamani kwasababu waliolieta bungeni kwa mara ya kwanza walidai kuwa unaboresha sheria iliyopo sasa ya vyama vya siasa, lakini ukweli ni kuwa muswada huo umetungwa ili kufifisha Demokrasia hapa nchini, “ amesema Zitto.

Aidha mapungufu muswada huo kufanywa kuwa jinai matendo yafwanyayo na vyama vya siasa, kutoa madaraka makubwa kwa msajili wa vyama vya siasa, kumpa kinga masajili wa vyama vya siasa na watumishi wa ofisi yake dhidi ya mashtaka na kuingilia uhuru wa vyama kuijiendesha.

Vyama 10 vilivyoungana kupingwa Muswada huo ni Chama cha ACT-Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Chama cha Kijamii (CCK), Chama cha Democratic Party ( DP), Chama cha NCCR MAGEUZI, National League for Democracy (NLD) na Chama cha United People’s Democratic Party (UPDP).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles